Simba walienda uwanjani kutafuta sababu ya kugoma kucheza, waadhibiwe tu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Baada ya kukikagua kikosi chao na kile cha Yanga, Simba walijua kuwa hawako tayari kucheza derby na kufungwa tena na yanga kwa mara ya 5 mtawalia, ila hawakujua wataanza vipi kuacha kupeleka timu uwanjani siku ya mechi. Baada ya kutafakari sana wao wenyewe na kuwasiliana na baadhi ya wajumbe walioko kwenye bodi ya ligi ambao ni Simba allies, ndiyo wakaja na mpango huu wa kwenda uwanjani usiku bila kutoa taarifa pahala pooopooote pale ili wakute jambo litakalowapatia sababu (nyepesi) ya kugomea mechi.

Baada ya kukuta geti la uwanja limefungwa hawakutaka kuhangaika na kupata maoni na ushauri kutoka uongozi wa uwanja (BMT, Wizara), TFF/Bodi ya ligi wala vyombo vya dola (kamanda wa polisi Dar) ingawa uwezo wa kufanya hivyo walikuwa nao. Hawakutaka kupata maoni ya watu hao kwasababu wangesababisha geti lifunguliwe na kukosa hoja ya kugomea mechi.

Ingawa kanuni ipo ya kuruhusu timu ngeni kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa mechi siku moja kabla ya mechi lakini kanuni hii kwa hapa kwetu Tanzania ni optional; sio mandatory (lazima) kwamba lazima timu zote kwenye ligi zifanyike mazoezi ya mwisho la sivyo mechi itaahirishwa. Kwanini simba mara hii waliigeuza kanuni hii kuwa ni mandatory (pre-requisite) ya kucheza mechi na Yanga tarehe 8?, Je, Simba huwa mechi zake zoooote ilizocheza huko nyuma zimetanguliwa na kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa mazoezi kabla ya mechi? Kama sio, kwanini iwe ni lazima safari hii kwenye mechi hii?

Kulikuwa na dhamira (maandalizi) ya Simba kugomea kupeleka timu uwanjani. Yanga ipewe points zake 3 na simba lolote liwakute kwa mujibu wa kanuni za ligi na sheria za nchi kwa walioathirika na uwahirishwaji wa mechi.
 
Simba walifika saa moja kasoro kadhaa, wakaondoka saa tatu usiku

 
Simba hawana hoja
Walifanya pre match meeting na kusema wamejiandaa na wako tayari Kwa mchezo
Wanasema eti walizuiwa na mabaunsa wa Yanga.
Toka lini Yanga ikawa na watendaji mabaunsa ?
Hao mabaunsa wangezuiaje msafara wa Simba wenye escort ya police?
Hao mabaunsa waliowazuia wawataje Kwa majina tuone kama ni watendaji wa Yanga.
Simba waliandaa upenyo wa kukimbia mechi
 
kwenye pre-match meeting sio simba wala mamlaka ya mpira waliowahabalisha watu na waandishi wa habari kuwa kutakuwa na pre-match uwanja wa Mkapa kwa wanaopenda kwenda kuhudhuria mazoezi hayo kama kawaida.
 
Kaka unakua kama mgeni kwenye Mpira. Kuna muda ushabiki weke pembeni. Leo unahoji suala la mabausa kwa Simba na yangu. N
 
Kaka unakua kama mgeni kwenye Mpira. Kuna muda ushabiki weke pembeni. Leo unahoji suala la mabausa kwa Simba na yangu. N
Sasa wana uhakika gani kuwa wale mabaunsa ni watumishi wa Yanga?

Yanga haimiliki uwanja wa Taifa
Yanga alikuwa mwenyeji kiitafaki tu hana mamlaka ya kulinda uwanja wala funguo za mageti
 
Ni jambo la kutafakari sana kuona Aston Villa ikicheza robo fainali za UEFA wakati Man United haijawahi kushiriki hata kwenye hatua ya mtoano tangu kuondoka kwa Sir Alex Ferguson
 
Kaka kuna baunsa mbele ya kikosi cha polisi FFU na maji ya washawasha, farasi, mbwa na mabomu ya machozi kuwatanya mabaunsa? kwanini jeshi la polisi halikuhusishwa?
 
Msiongeigopa Simba simple tu msingewazuia kufanya mazoezi.

Hizi pumba zote zisingekuwepo na Simba wasingekua na base ya kugomea mechi.

Over
 
Hakika aliewaita utopwinyo aliwaza mbali sana
 
Hicho kikosi cha Yanga ndio kilichopigwa 3-1 na Tabora au kile kilichoshindwa kuwafunga JKT?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…