Simba wamebaki kulilia huruma za Mh Rais

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Baada ya Mh Raisi kutangaza dau nono la Milioni 5 kwa kila goli na pasipo na shaka Yanga ikionekana kwenda kukausha kibubu hicho Simba nao wameibuka wakitaka kupewa viti maalumu i mean wanataka fedha za mama kupitia viti maalumu yaani sandakalawe.

Hayo yote yameibuka baada ya kuona mpaka sasa wamefunga goli 2 tu na kuondoka na Tsh milioni 10 huku yanga wakikaribia milioni 50 wakiongozwa na Wanaojiita wachambuzi wao wa kimchongo wameanza kulia kwenye vyombo vya habari hata humu jf wakitaka fedha za Sandakalawe.

Agenda yao mfu ni kwamba wao wanajiona washabeba kombe la mabingwa na kutaka Raisi awape fedha zaidi ya Yanga na kusahau Mh Rais katoa hisani tu.

Suala la kujiuliza je hata Mh Rais angesema ndio anawapa million 100 kwa goli je wangeweza kupindua kile kipigo cha goli tatu kutoka kwa Morroco hawa jamaa wametoka kuwa serious na mpira na kuwekeza kwenye porojo za uwongo uwongo, sio ajabu waliletewa Manzoki kama mgombea na mpiga kura.

Simba pambaneni na sio kutegemea Vitonga kama shirikisho kwepesi mbona mlitumia uchawi pale kwa madiba.
 
Milioni tano wakati inaenda Super League na pesa ya maandalizi ni zaidi ya bilioni 4..mtoa Uzi zinakutosha mwenyewe tu
 
Milioni tano wakati inaenda Super League na pesa ya maandalizi ni zaidi ya bilioni 4..mtoa Uzi zinakutosha mwenyewe tu

Hahaa inaenda lini masta mbona mnalilia sasa huku street hapo ulipo jipige kifua mara 3 kama ulifurahia ujio wa manzoki siku ya uchaguzi jiulize hivi manzoki alikuja kama nani mgombea binafsi au then shushia na maji mengi halafu lala zako kiroho safi.
 
Simba ni
WAPUMBAFFFF,
MALOOFA!!
 
Sasa we unadhani simba wanawaza hvyo Visent uchwara wakati Caf champions league wana pata hela nyingi kuliko wale walio kwenye Caf confederation cup.
 
Yaani simba awaze ml 5 wakati CAFCL anakunja bln 1.5 halafu yule wa kombe la losers anapata ml 800? ?
 
Sasa we unadhani simba wanawaza hvyo Visent uchwara wakati Caf champions league wana pata hela nyingi kuliko wale walio kwenye Caf confederation cup.
Sasa mbona mnalialia kutafuta huruma [emoji3][emoji3][emoji3]

Mkiongozwa na mcha-[emoji238] wenu Jemedari[emoji3]

Sent from my Infinix X689C using JamiiForums mobile app
 
Kuna fine line kati ya kutoa mtazamo wenye mahitaji fulani fulani ndani yake na kuonekana unalia ulia lia.

Ila kwa hili, Wachambuzi na Mashabiki wanaweza kuwa na point ndani yake, wasikilizwe. Ila sio lazima watimiziwe.

Why wasikilizwe?
1. Haya ni mashindano tofauti, yenye magnitude/ushindani tofauti.
(Najua Yanga wanaweza wasiamini, ila hii Safari ya CAFCL mapema kabisa ili washinda).
To Rub some more salt into Yanga's Wound. Ni miaka 24-25 hamjafanikiwa hata kuingia hatua Makundi huku CAFCL.

Why sio lazima watimiziwe.

Hii Mil.5 per goal sio salary, sio bonus ya timu bali ni reward (Just a recognition of achievement). Hii siyo haki ya mtu yeyote, Madame President atoe asitoe hakuna ataye complain. So, ameamua Mil. 5 Per goal ibaki hivyo na itabaki hivyo.

N.B. Haya maneno hayatoki kwenye uongozi timu, bali ni mitazamo ya wachambuzi na mashabiki tu.

Ushauri: Kama unaona mil.5 ni ndogo, mpige mtu goli nyingi upate pesa nyingi(The more you score, the more you receive reward).

In Tanzania: Yanga may be a big fish🐡 but Simba is whale🐋
 
Baada ya Mh Raisi kutangaza dau nono la Milioni 5 kwa kila goli na pasipo na shaka Yanga ikionekana kwenda kukausha kibubu hicho Simba nao wameibuka wakitaka kupewa viti maalumu i mean wanataka fedha za mama kupitia viti maalumu yaani sandakalawe.
Mkuu, ukiona zawadi ya timu zinazoshiriki Klabu Bingwa (CAF CL) kuanzia nafasi ya kwanza hadi ya nne katika kundi, pengine utajua kwamba milioni tano tano ni hela ya viungo vya mboga (sio mboga)



Kwa hiyo hadi sasa Simba hata akishika mkia katika group lake ana uhakika wa kupata US $550,000 sawa na shilingi za Tanzania 1,265,000,000/= (Bilioni Moja Laki Mbili na Elfu Sitini na Tano tu). Hiyo ni sawa na kusema Simba itapata hela ya magoli 263 kama utachukua kwamba kila goli ni sh. milioni tano. Kwa hiyo hela zinapokelewa kama heshima tu lakini nimekupa hiyo hesabu ili uangalie kipi ni kipaumbele, ushindi ili ukachukue mahela zaidi au magoli ili upate milioni tano tano!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…