Simba wamecheza chini ya kiwango, kuna kitu

Simba wamecheza chini ya kiwango, kuna kitu

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Nasema wazi kabisa kwa mchezo wa jana tulipaswa kuadhibiwa.

Wachezaji wamecheza chini ya kiwango. Imefika mahali ninaanza kushawishika huenda kuna kitu zaidi ya mchezo.

Shaffi Dauda anaishi na siri. Hii michezo huwa ni fursa kwa watu wengi sana hasa wapiga dili. Ninaona mipango ya Simba kuja kushinda goli 3 -1 kwa Mkapa tuendelee na stori tulizozizoea za kutolewa kishujaa.

Liko jambo na safari ndio imefikia mwisho kwa Simba.
 
Mmmh Shafii Dauda ana influence gani mpk umhusishe
hii hapa uzuri waliohusishwa hadi leo wako kimya na klabu imekaa kimya fungu la GSM HAWA vijana wawili wanalo hadi leo watakataa hata milioni 100 ,mia za kazier chiefs wandishi wa habari wote wameifata simba huko hadi mzee wa deal SHAFFIH DAUDA?DAH

SHAFF8IH ZIMBE KAPOMBE.PNG
 
Alright alright sasa naweza kukubaliana na hoja yako.
balaa sana ndugu haya tuyaangalie juuu juuu tu we acha tu soo sana aiseee namba mbili na namba tatu zetu zinatembea na advance ya GSM shaffih dauda ana ushahidi halafu klabu imekausha tu kwamba yataisha juu kwa juu na jana zikaamua kuvujisha bado yanga nao kutupiga tano
 
balaa sana ndugu haya tuyaangalie juuu juuu tu we acha tu soo sana aiseee namba mbili na namba tatu zetu zinatembea na advance ya GSM shaffih dauda ana ushahidi halafu klabu imekausha tu kwamba yataisha juu kwa juu na jana zikaamua kuvujisha bado yanga nao kutupiga tano
Hivi nyie ni wakina nani mpaka msifungwe,kwa hiyo unataka kutuambia nyie mkishinda ndio michezo mnayofanyaga ya kuhonga timu pinzani sio?
 
Simba hawakucheza chini ya kiwango kabisa.

Watu wengi wanachukulia Simba kutokufunga ndo wamecheza chini ya kiwango angalia ni timu ipi iliposes mpira sana kama siyo simba?

Tuache unafiki

Simba walizidiwa mbinu na tatizo jingine simba walikaa muda mrefu bila mechi tofauti na wapinzani wenzao.

Na hata wanapokuja watu wanasema korona imeisaidia sana simba kufika hapo muelewa sana maana wakati ligi yetu ikiendelea mataifa mengi walikuwa hawachezi

Tatizo ni plan ya simba, simba wanastaili moja tu ya kucheza yaani viunngo wegi .

Wakijua hasa kuwa hatari wanayoweza kuipata ni kurehusu kapombe apande hivyo wakampangia jamaa mwenye nguvu, na kumfanya kapombe asipande, jamaa akagundua siyo kapombe tu Bali hata shabalala ndo akaamua kumwingiza mchezaji mwingine dkk ta 35 Tu akimpa jukumu la kumbana asipande .

Simba ikibanwa mafullbeki wake hawawezi tokea pembeni watataka kupitia Kati na jamaa walikuwa wameshawawin katikati kabisa .

Jamaa waliwaacha wacheze mpiara wao wakatumia counter attack kuwamaliza .

Walikuwa na nidham ya mchezo Sana walipokuwa hawana mpira walirudi wote au kuacha mtu mmoja mbele walikuwa wanapanua uwanja ili kueanyima Simba kukimbia na one touch zao za karibu karibu.


Simba wamecheza sana lkn walizidiwa mbinu na kaizer chiefs
 
Hivi nyie ni wakina nani mpaka msifungwe,kwa hiyo unataka kutuambia nyie mkishinda ndio michezo mnayofanyaga ya kuhonga timu pinzani sio?
wewe ni muhusika wa kusinya hizo pre contarct au msemaji wa li chambuzi nguli kabisa nchi hii?KWA NINI KAPOMBE NA ZIMBWE JR HADI LEO WANATEMBEA NA HELA ZA ADVANCE ZA GSM ?HUU UZI NILIWEKA HAPA LONG TIME TU KAMA MWEZI JANA UMEANZA KUONYESHA MATOKEO YAKE BADO MECHI YA UTOPOLO TUTAONA MENGI
 
Simba hawakucheza chini ya kiwango kabisa.

Watu wengi wanachukulia Simba kutokufunga ndo wamecheza chini ya kiwango angalia ni timu ipi iliposes mpira sana kama siyo simba?...
Simba wamecheza? wamecheza nini, zile pass za kupigiana nyuma mbele nyuma mbele ndio kucheza? wapi umeona hata kum test kipa wa Kaizer au kuwazunguka beki za Kaizer.

Nachukia sana kuona team inafungwa 4 halafu anakuja mtu anasema lakini tume poses mpira ni malengo na mpira ni magoal sio kumiliki mpira halafu umiliki wenyewe hauna maana yoyote mipira yote waliyotaka kupiga kwenye 18 wale Kaizer wali deal nayo yote.

Kaizer ni warefu na wakatumia silaha ya urefu wao na uhakika Simba hawakufanya homework kuhusu hawa jamaa nguvu zao ziko wapi. Simba jana wamecheza mpira mbovu kabisa na kiwango cha jana ndio kile cha zamani cha tano tano.
 
Mnatafuta watu wa kuwaangushia jumba bovu na kwa vile mnawachukia watanzania wenzenu Shomari na Mood mmeamua kusemea mbovu ili waonekane wamechomesha. Sababu ziko wazi na ni mbili au tatu tu na katu haziwahusishi Kapombe na Zimbwe peke yao.
1.Kutoheshimu mpinzani.

Kwa hili Simba walifeli ndani ya dk 10 tu za awali wakicheza na timu kubwa Afrika utadhani wanacheza na Dodoma jiji.
2.Lack of second & third plans.

Angalia aina ya magoli waliyofungwa yanvyofanana, angalia jinsi walivyotumia mbinu zilezile kutaka kupenya ngome kwa style iliyofeli tangu mwanzo.

3.Beki mbovu ya kati.
Hapa ndo mnaposhindwa kusema ukweli. Simba wamekuwa na ugonjwa huu muda mrefu na mashabiki wake mnajaribu kuufunika sijui kwa faida ya Nani? Wawa kafanya makosa kuliko mchezaji yeyote jana uwanjani, Onyango kakosa utulivu kama beki anayepaswa kujua mtindo wa adui na kujipunguzia au kujiongezea majukumu. Lakini pia ni hawa wawili wanaotakiwa kufuta makosa ya wachezaji wengine wote kwani wakiacha kosa liendelee timu inaadhibiwa.

Mfano wa ubovu wao;
Angalia upya goli la NNE.
 
Kufungwa ndio kujifunza.
Kumbukeni hii ni Robo Fainali Club Bingwa Afrika.
Tutayafanyia kazi mapungufu.
 
Kukaa bila kucheza mechi ndio tatizo kubwa kama umewai kucheza soka utaelewa ilo.na walituzidi mbinu za uharaka kufika kwenye nox letu

Gomez kila muda alikuwa anapiga kelele kuwa twende kwenye box lao ila wapi, tujipange mechi ijayo
 
Back
Top Bottom