Simba wamekuwa wapole, na adabu juu!

Simba wamekuwa wapole, na adabu juu!

SALOK

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2011
Posts
3,364
Reaction score
2,001
Asubuhi ya leo, Feb 19, 2023 Mashabiki wa Simba, mashabiki wa hovyo kuwahi kutokea Duniani, mashabiki jeuri, wajivuni!

Mashabiki wanaojua kuvimba kwa sifa wasizokuwa nazo pale litimu lao bovu linapobahatisha kushinda uwanja wa nyumbani kiuchawi uchawi.

Ghafla wamekuwa wapooole! wenye nidhamu na heshima na taadhima!

Leo asubuhi kila ninapokatiza kukutana nao nasikia.. “Habari za asubuhi Brother, vipi familia mmeamkaje! Sisi pia ni wazima tunashukuru!!”

Ahsante sana Raja kwa mafunzo mujarabu kwa mtoto mtukutu.

Tukutane baadaye muone boli linavyochezwa!!!
 
Robo tatu ya wachezaji wa Simba including Manula hawastahili kuwepo/kucheza Simba......
Hata ungemleta Klopp, Mourinho, Guardiola wote hao wakae pale benchi kwa wachezaji waliopo Simba hii, wallahi hawatoboi....

Ni vile ligi yetu nayo ni ya kimagumshi sana...ndo maana tumesubiri Raja aje atuoneshe panapovuja
 
Ni swala la muda tu tutakuwa tunachekana wote humu.
Kuchekana nasi Utopolo hapana usijifaariji Mkuu! Nyie kufeni kivyenu sisi UTOPOLO tunajua tutashinda!

Raja watu WABAD sana wamefumua mshono wa Horoya kama tulivyotarajia maana Simba ishakuwa Paka siku hizi!! Umri wa kocha na umri za wachezaji kina Babu Onyango zimepishana two years tu!!

Mavuvuzela yenu kelele kibao mitaani mkishinda huwa mnatuamshia vichanga vyetu sijui eeeh kidedeaaaa wengine Wana mizuka wanaitikia kwa nguvu eeh kidedeaaaa leo mavuvuzela hamna! Wote kimyaaaa!

Vijana wanasimba bodaboda kelele kibao honi mji mzima Fujo kama zote sifa kibao mikogo na mbwembwe za kuendesha boda boda kwa tairi moja la nyuma , Wote kimyaaaa!! majezi ya Simba yamekuwa mazito mitaani leo hamna, wote kimyaaaa!

Vijana wanasimba Leo wanatusalimia wazee kwa heshima wanasema Mzee shikamoo, vipi habari za Jumapili, vipi familia hawajambo wote , sie tupo tu Mzee! Ha ha ha, Sasa Jana wangeshinda adabu zingekuwa kabatini asubuhi bila salamu wangesema "Mzee uliona Jana Pira Biriani? Mi Huwa nakwambia Chama JR ni sawa na timu yenu nzima ya Utopolo!!" Wangeuliza hivi Mzee huko utopoloni kwenu wote hamjitambui ama sivyo!

mambo murua kabisa Jiji lote kimyaaaa kahawa zetu zinashuka taratibu kweli ni Raha mustarehe Kwa utopolo sote!
 
Bado Simba ana nafasi ya kwenda robo fainali, waliobaki tunawamudu tushindwe wenyewe.
 
Robo tatu ya wachezaji wa Simba including Manula hawastahili kuwepo/kucheza Simba. Hata ungemleta Klopp, Mourinho, Guardiola wote hao wakae pale benchi kwa wachezaji waliopo Simba hii, wallahi hawatoboi.

Ni vile ligi yetu nayo ni ya kimagumshi sana...ndo maana tumesubiri Raja aje atuoneshe panapovuja
Labda wewe tu ndo ulikua huoni madhaifu ya Simba fwatilia nyuzi za humu nyingi watu wanaongea madhaifu ya Simba lakini mnajifanyaga hamuoni mnakimbilia kujadili mikataba ya Feisal na Sportpesa
 
Asubuhi ya leo, Feb 19, 2023 Mashabiki wa Simba, mashabiki wa hovyo kuwahi kutokea Duniani, mashabiki jeuri, wajivuni!
Mashabiki wanaojua kuvimba kwa sifa wasizokuwa nazo pale litimu lao bovu linapobahatisha kushinda uwanja wa nyumbani kiuchawi uchawi....
Sawa mkuu ngoja tuone badae itakavyokua maana hawa jamaa nimapacha
 
Wangeshinda, ungeona wakivamia ukurasa wa CAFCLCC na wa Raja kwa kuongea maneno ya ovyo. Ila saivi CAFCLCC wamewekwa highlight na matokeo kumekuwa kimya kumetulia.
Wamekuwa wadogoo!!
Robo tatu ya wachezaji wa Simba including Manula hawastahili kuwepo/kucheza Simba......
Hata ungemleta Klopp, Mourinho, Guardiola wote hao wakae pale benchi kwa wachezaji waliopo Simba hii, wallahi hawatoboi....

Ni vile ligi yetu nayo ni ya kimagumshi sana...ndo maana tumesubiri Raja aje atuoneshe panapovuja
Raja ametusaidia kwakweli..
 
Labda wewe tu ndo ulikua huoni madhaifu ya Simba fwatilia nyuzi za humu nyingi watu wanaongea madhaifu ya Simba lakini mnajifanyaga hamuoni mnakimbilia kujadili mikataba ya Feisal na Sportpesa
Chief, hakuna mahali nimesema Simba Haina madhaifu...yapo yanajulikana na kama unavosema yamejadiliwa sana ila Viongozi nao ni sehem ya madhaifu pia. Ndiyoo maana walishindwa kumsajili Manzoki ila wakamleta kwenye uchaguzi....upumbavu wa kiwango Cha juu sana

Hilo la Fei, linajadiliwa na Kila mtu sio wasimba pekee
 
Kuchekana hapana usijifaariji, Nyie kufeni kivyenu sisi UTO tunajua tutashinda! Mavuvuzela yenu sijui eeeh kidedeaaaa hamna! Vijana wanasimba bodaboda Wote kimyaaaa!! majezi ya Simba mitaani leo hamna, mambo murua kabisa Jiji lote kimyaaaa kahawa zetu zinashuka taratibu kweli ni Raha mustarehe Kwa utopolo sote!
Masikini Kijana vunjaprice, yale matambara aliyoagiza itabidi ayauze kwa bei ya sagura sagura!!
 
Back
Top Bottom