Simba wameponzwa na kushinda mechi zote za ugenini

Simba wameponzwa na kushinda mechi zote za ugenini

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mwalimu wa Simba amekosea sana kuwataka wachezaji wake wacheze kufa na kupona ili kushinda kila mechi hata zile zilizochezwa ugenini kwenye viwanja vibovu sana. Baadhi ya viwanja vya mikoani ni vibovu sana kufaa kuchezewa mpira wa miguu. Ubovu wa viwanja hivi huwa unatumiwa vibaya na timu za mikoani kujipatia pointi kutoka timu kubwa hasa za Dar es Salaam ambazo zina professional wengi na viwanja vizuri. Timu kubwa zenye wachezaji professional lazima zicheze chini ya kiwango kwenye viwanja hivi vibovu ili kuwalinda wachezaji wao wasiumie na kuumizwa wanapocheza na timu za mikoani kama Ndanda, Stendi, Mwadui, Majimaji, n.k kwenye viwanja vibovu kama Kambarage. Mwalimu makini atawapunzisha wachezaji wake muhimu kwenye mechi kama hizi au kuwachezesha kwa muda mfupi tu ili kuwalinda waziumie na kuumizwa. Nina uhakika mimi kuwa wachezaji wa Simba wengi ama wameshachoka au wana maumivu mbalimbali kwenye viungo vyao kutokana na kucheza kwa nguvu mechi zote hata kwenye viwanja vibovu, na matokeo yake umeyaona sasa wachezaji wanacheza chini ya viwango hata kwenye viwanja vyao vya nyumbani, wameshindi kuendeleza mwendo wao kazi.

Azam na Yangu makocha wao sio wajinga kuhuruhu sare au hata kufungwa kwenye viwanja vibovu, hii inawasaidia kuwalindinda wachezaji wao na majeraha yanayoweza kusababishwa na kukamiwa kwenye viwanja vibovu. Simba wasipoangalia hata nafasi ya pili hawataiona itakakopitia.

Siku zote Mzungu ni Msungu tu na Mweusi atakuwa mweusi tu, Omog ameshindwa kufahamu kuwa kinachotakiwa ni kuchukua kombe na sio kufunga kila mechi kwenye ligi.
 
Ulitakiwa uyaseme hayo kama ushauri kabla ya hizo mechi kuchezwa.
 
Back
Top Bottom