Simba wana mgao kwa Samatta kwenda Aston Villa?

Simba wana mgao kwa Samatta kwenda Aston Villa?

Ngoja tusubiri wajuaji: ila ni kama nakumbuka vile waliwahi kupiga mshiko fulani hivi wakati samata anahamishiwa Genk kutoka mazembe
Wala hujakosea mkuu walishachukua chao, anayeweza kudai hapo ni TP Mazembe!
 
Ishu sio kumharibia samata ishu mkataba unasemaje? Kwa nilivyosikia hapo mwanzoni kuwa kila samata anapouzwa simba ina % yake kutoka kwa timu inayopokea mzigo kwahiyo simba hawataidai AV wataenda kudai Genk
Genk hawamjui simba, anajuana Genk ni TP Mazembe kwa hiyo kwenda kumdai Genk simba watakuwa wanapoteza muda! Wasubiri huruma ya TP Mazembe!
 
Mkipata huo mgawo semeni tuone.
Vitu vidogo hamtaki kuelewa.. Shida iko wapi?
Wewe ndio hutaki kuelewa hicho kipengele kilielezewa toka mbwana anaenda mazembe kuwa mara zote atakazouzwa simba wana mgao, nikwambie tu mimi sio simba fan
 
Genk hawamjui simba, anajuana Genk ni TP Mazembe kwa hiyo kwenda kumdai Genk simba watakuwa wanapoteza muda! Wasubiri huruma ya TP Mazembe!
Mzee usibishe vitu usivyovijua wakati samata anauzwa Genk hao Genk walipewa taarifa kuwa kunakipengele hicho, kwa taarifa yako mazembe ndio hawana mgao hapo
 
ni suala la mkataba, alipotoka simba kwenda mazembe labda kama kulikuwa na kifungu kwenye mkataba wa mauziano.
kuwa mazembe mkimuuza simba tupate 10% ya bei.

sasa mazembe wanapomuuza kwenda genk, wao ndio wanaingia kwenye mkataba wa mauziano na genk na kama waliweka kipengele basi mazembe watapata % ya mauzo ya samata kwenda astoni villa.

nafikiri pia hivi vifungu utegemea bei ulipouza mchezaji, kama bei ya wastani basi vipengele vya kunufaika vinawekwa lakini kama ilikuwa bei kumalizana haupati kitu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mabata fc, a.k.a nyuki ndegelec kwasukwasu utayajua tu!!
...yana comment ulevi yaliyoupata baada ya kunywa glass 3 za juice ya miwa iliyochanganywa na Mo linga energy!!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Samata aligoma kufanya mazoezi simba baada ya kutotimizia ahadi ya kupewa gari, ndio akaenda tp mazembe, hiyo 10% haipo.
Ikawaje Simba wakapewa 20% ya Mazembe kwenye ada ya Genk?

Akili zako umeziweka kwenye kiungo kipi nje ya kichwa?
 
Kwani Aden Rage anasemaje?
Naamimini ana nafasi nzuri kutoa elimu kwa watu wake anaowajua fika
 
Tujuzane kidogo.

Kila kitu kinategemea na mikataba/kandarasi iliyoingiwa na club hizo kipindi cha uhamisho wa mchezaji.

Kuna kitu kinaitwa 'sale-on clause' ambacho huwekwa kwenye mikataba (sio lazima) wakati wa kuuziana wachezaji baina ta team na team. Hii huipa uwezo klabu kuwa na haki ya kupewa kiasi/asilimia kadhaa cha/za pesa kutokana na mauzo ya mchezaji waliemuuzia klabu nyingine pindi mchezaji huyo atakapouzwa hapo baadae kwenda klabu nyingine (third party)

Katika kipengele hicho lazima klabu ziafikiane conditions za ku trigger/activate clause hiyo ili kila mmoja kujiweka katika 'win-win situation'.

Kwamfano unaweza kukuta labda klabu zinakubaliana kwamba kama mchezaji akiuzwa kwa kiasi cha pesa kinachozidi labda TShs 10, 000/- basi klabu yake ya zamani watapewa asilimia 5 ya mauzo. Kama akiuzwa kwa Tshs 100, 000/- basi klabu ya zamani watapewa asilimia 10 ya mauzo. (Hiyo ni mifano tu ili tuelewane).

Conditions nyingine ni kama ranking ya league atakayouzwa. Mfano labda mchezaji akiuzwa kutoka Africa kwenda Ulaya rate ya sale on clause inaweza kuwa kubwa kuliko kama akiuzwa klabu ya Africa kwenda labda Uarabuni au hapa hapa Afrika.

Conditions zipo nyingi ikiwa ni pamoja na ku consider kuwa mchezaji anaweza asi realise potential yake hivyo thamani yake kwenye transfer market ikapungua, au akapata career ending injuries n.k. Hivyo klabu lazima pia zikubaliane kama ikitokea hivyo malipo yanaweza kutokuwepo n.k.
Uko sahihi kabisa. Sasa kwenye hili sakata mnyama atalamba 20% atakachopewa Mazembe?
 
Hii sasa imekuwa debate ya vipofu.

Hakuna mwenye uhakika wa kuwepo kipengele cha kuwaruhusu Simba kupata chochote..
 
Uko sahihi kabisa. Sasa kwenye hili sakata mnyama atalamba 20% atakachopewa Mazembe?
Kwa hilo la Mnyama kupata mgawo sijui kwasababu sijui chochote kuhusiana na kandarasi walizoingia na Mazembe wakati wanauziana hiyo mchezaji. Lakini kama mtu wa ndani amethibitisha kuwa kutakuwa na mgawo nadhani inaweza kuwa kweli na ndio maana nimeeleza kuhusu hiyo clause ili watu wajue kuwa inawezekana kweli Simba kupata mgawo endapo tu hizo clause zilikuwemo kwenye makubalino wakati wakimuuza Mazembe.
 
Back
Top Bottom