Wakuu,
Yapo mengi tunaweza kuyataja kama mapinduzi ya uendeshaji timu kisasa yaliyoanzishwa na Simba. Leo ningependa kutaja eneo moja ambalo miaka michache ijayo tutaelewa hii project.
Simba imeamua kuwekeza kwa makocha wazawa! Seleman Matola amecheza muda mrefu Simba na sasa ni kocha wa muda mrefu pia Simba! Matola amefanya kazi na makocha wengi wa kigeni na kupata exposure kubwa yumkini kuliko kocha yeyote mzawa nchi hii.
Msishangae hata kelele za mashabiki hazimuondoi Matola ni sababu Simba ime invest sana kwake na haipo tayari hayo matunda wakale wengine. Kwenye inner cycle ya Simba wanasema inaweza kufukuzwa hata timu nzima ila sio Matola.
Matola amepelekwa shule apate leseni ya juu ya ukocha na ukiongeza na exposure aliyokwishapata atakuwa moto sana.
Legend mwingine ni mshambuliaji wa zamani Musa Hassan Mgosi! Huyu ametumika kwenye nafasi mbalimbali za ukocha na sasa amepelekwa USA kwa mafunzo zaidi.
Kuonesha Simba ipo serious wakamchukua Juma Mgunda kocha mwenye experience kubwa lakini aliyekosa exposure hasa kwenye management ya Technical team na benchi pana kama la Simba linahitaji uzoefu kuli manage.
Kwa ubora wa Mgunda muda atakaokaa na huyu kocha mpya atavuna mengi na baadae kwa kusaidiana na Matola tusishangae wakafanya makubwa! Mgunda alipata exposure ndogo Taifa Stars sababu programme zao ni fupi na hawana Technical Team kubwa kama ya Simba.
Hili tuweke unazi pembeni Simba wanapika watu watakaokuja kusaidia sana Taifa na hata baadae kufundisha soka nje ya mipaka yetu.
TFF wasingehangaika kutafuta kocha nje, wampe timu Mgunda na wasaidizi Matola na Minziro kwa uzoefu wao na wachezaji wetu tutapata matokeo walau mazuri kwa kuanzia.
Hongereni sana Simba Sports Club. Haya Uto nyuzi zingine za kizalendo tuungane bana [emoji1787]
Sent from my SM-A315F using
JamiiForums mobile app