Simba wanamkosa kipa aina ya Juma Kaseja

Rogers luyangi

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2014
Posts
552
Reaction score
948
Kwa msimu wa pili mfululizo Simba wanatolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika hatua ya Robo Final kwenye mashindano ya CAF.

Nyakati kama hizi ndio unakumbuka kipindi ambacho Juma K. Juma akiwa langoni ilikua ni ngunu sana kupigwa penati tano (5) bila kucheza walau penati moja.

Simba wanahitaji kipa aina ya Kaseja au ujuzi wake wakufundisha makipa pale ndani ya timu ya Simba.
 
Simba wanahitaji kipa wa futi 6 kama Emiliano Martinez wa Argentina. Kipa mrefu akiruka ile "wingspan" yake na urefu wa miguu unasaidia kufunika goli zaidi kuanzia kwenye mikono hadi miguuni kote inakuwa ni kinga. Pia mipira ya krosi na kona yote anakuwa na faida zaidi ya kuidaka.

Penati ni ufahamu wa saikolojia zaidi kwa jinsi unavyoweza kumdanganya mpigaji ila kuna nyakati nyingi urefu unasaidia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…