Wildchild
JF-Expert Member
- Aug 29, 2018
- 19,411
- 21,938
Ukiona hivyo janja janja mingi.unakuwaje na wachezaji wengi bora na wenye viwango halafu bado hawako organized?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukiona hivyo janja janja mingi.unakuwaje na wachezaji wengi bora na wenye viwango halafu bado hawako organized?
kweli kabisa wanacheza kiwango kibovu, yani hakuna timu ya kuifunga yanga pale labda iwe bahati nasibuNime angalia mechi walio cheza Jana na Azam, Simba bado wana tatizo lilelile hawajajirekebisha, mimi sio mtaalamu wa mchezo wa mpira lkn kwa mtazamo wangu wa kawaida Simba inakosa mbinu inayo faa ktk ushambuliaji, ushambuliaji wao hauna nguvu ya kuzalisha magoli kama ikivyo kwa wapinzani wao...
wana bahatisha bahatisha tu unakuta mechi moja ya ovyo ovyo huko wanapiga goli saba, mechi za muhimu kama derby bado kikosi hakiko serious kabisa kulingana na uzito na pressure ya derbyMnafurahisha sana, eti simba haina mbinu ya ushambuliaji yenye kuzalisha magoli. Hapo hapo Simba hiyo hiyo ndo inaongoza kwa kufunga magoli mengi ligi kuu ..
Timu yenye magoli 74 inasemwa ina safu dhaifu ya ushambuliaji[emoji2369][emoji2369][emoji2369][emoji2369][emoji2369]Nime angalia mechi walio cheza Jana na Azam, Simba bado wana tatizo lilelile hawajajirekebisha, mimi sio mtaalamu wa mchezo wa mpira lkn kwa mtazamo wangu wa kawaida Simba inakosa mbinu inayo faa ktk ushambuliaji, ushambuliaji wao hauna nguvu ya kuzalisha magoli kama ikivyo kwa wapinzani wao.
Simba wasipo badilika hiyo trh 25 wanachapwa tena.
sipendi Mnyama aadhirike tena.
Kwahyo unashaurije??Hayo magoli yasiwe yanahesabiwa?tatizo sio tu kuwa na idadi ya magoli au kufunga ila pia ni muhimu kuangalia ubora wa magoli waliyo funga, timu kubwa kama simba unafunga goli kama la mchezaji wa Ihefu kweli!!
Hiyo timu kweli ushambuliaji wake hauna nguvu. Hata ukicheki takwimu imeizidi Yanga kwa magoli machache sana ya kufunga. Goli 22 tu na Ameizidi Azam kwa goli 27 tu za kufunga.Nime angalia mechi walio cheza Jana na Azam, Simba bado wana tatizo lilelile hawajajirekebisha, mimi sio mtaalamu wa mchezo wa mpira lkn kwa mtazamo wangu wa kawaida Simba inakosa mbinu inayo faa ktk ushambuliaji, ushambuliaji wao hauna nguvu ya kuzalisha magoli kama ikivyo kwa wapinzani wao.
Simba wasipo badilika hiyo trh 25 wanachapwa tena.
sipendi Mnyama aadhirike tena.
Si ndio hapo sasa. Sijui wanashindwaje kuwa kama Yanga wakiamua droo wanakuwa "constant". Wachezaji wakiamua kuwa watovu wa nidhamu wanakuwa "constant"tatizo la simba ni Maji kupwaa.....Maji kujaa.
Ubora na viwango vyao lazima viwe "constant" sio leo hivi kesho vile.
Kweli kabisa.... Kama yule Waziri Junior wa Simba alivyokosa magoli ya wazi kwa Ihefu juzi.Simba hawana pressing yenye nguvu na kuzalisha bao
Timu kama simba inakosa open chance inayo muwezesha mchezaji ku score...anakosa anabaki kupanua mdomo na kushika kichwa!! zaidi hata ya mara tatu!! aghhh!
[emoji23][emoji23][emoji23]Umesema Simba haina mbinu ya ushambuliaji .
Okay Sawa Kwani ni timu Gani inaongoza kufunga magoli mengi kwenye ligi?
Ntajie timu moja Duniani iliyo "constant"tatizo la simba ni Maji kupwaa.....Maji kujaa.
Ubora na viwango vyao lazima viwe "constant" sio leo hivi kesho vile.
labda kama kila mwezi wanasajiliwa wachezaji wapya, lkn kama wachezaji wapo pamoja kila siku zaidi ya mwaka lazima wawe well organized,Ntajie timu moja Duniani iliyo "constant"
It is a simple question...Sasa wewe uitaje hiyo team iliyokuwa "constant" msimu mzima hapa dunianilabda kama kila mwezi wanasajiliwa wachezaji wapya, lkn kama wachezaji wapo pamoja kila siku zaidi ya mwaka lazima wawe well organized,
Kwani Hawa si wanasema Wana KIKOSI KIPANA!?Yani umeangalia mechi ya kikosi cha tatu umeandika na uzi ..
Mkuu umemaliza kabisa. Ni kweli kabisa Simba ndiyo timu yenye viungo bora kabisa na washambuliaji wakali kuliko wote ligi kuu lakini tatizo lao kubwa ni mizaha, kudharau baadhi ya mechi, kukosa umakini, kuridhika wakishapata goli mbili/tatu na nidhamu ya ukabaji kuanzia mbele (pressing). Viungo wa Simba wanatengeneza kwa wastani nafasi za wazi zisizopungua kumi (kutegemeana na mechi) kwa washambuliaji wao katika kila mechi lakini zinazotumiwa kwa usahihi ni mbili mpaka tatu. Kila siku nasema iwapo benchi la ufundi la Simba wangekuwa wakali na washambuliaji wangekuwa makini basi Simba ingekuwa inatoka uwanjani na goli tano mpaka saba kwenye mechi moja. Mfano mdogo mechi ya Coastal Union Simba walishinda goli 2 - 0 kwenye mechi ambayo viungo wao waliwatengenezea nafasi zaidi ya nane ukiacha kabisa zile ambazo mshika kibendera alizozizuia kwa off side anazozijua yeye mwenyewe binafsi.Mkuu unaweza kuwa upo sawa, Lakini je umetazama takwimu za mabao ya timu zote kwenye msimamo wa ligi?
Kama umetazama utaona kuwa Simba inawaacha wapinzani wake kwa mbali sana kwa wingi wa mabao!
Kwenye mechi ya jana Simba ilichanganya wachezaji wachache wa kikosi cha kwanza na wengi wa kikosi cha pili, na hivyo timu ilikosa muunganiko mzuri hasa kwa kipindi cha kwanza japo kuingia kwa NYONI na BWALYA kulibadili sura ya mchezo. Na ninadhani kocha alifanya hivyo makusudi kutopanga kikosi cha kwanza ili kutoa nafasi ya mapumziko kwa nyota wengi wa kikosi cha kwanza , lakini pia kutoa nafasi kwa wachezaji wa benchi kupunguza vitambi kwakuwa kama ni ubingwa tushabeba!
Kwenye mechi na Yanga , Simba ilikuwa na kasoro 3 za kiufundi, Kwanza waliingia kwa kujiamini sana kuwa walikuwa na asiklimia kubwa sana ya kushinda katika mchezo ule, wakasahau kuwa wapinzani wao nao wameshawapania!
Pili Simba waliingiza kikosi kwa kuanza mabeki wengi badala ya kunoa foward, washinde kwanza ndio wazuie kulinda ushindi. Matokeo yake timu ilishindwa kupandisha mashambulizi mbele na kujikuta wakishambuliwa wao mfululizo hadi mashambulizi hayo yakazaa goli!
Washambuliaji walikosa utulivu kila walipofika langoni mwa wapinzani wao, mfano ni mashuti manne yaliyopigwa ndani ya 18 na wachezaji Medie Kagere, Luis Mikison na John Bocco!
Kama foward ingekuwa na utulivu walikuwa wa kushinda mchezo ule achilia mbali mauzauza ya marefa kuwanyima penati mbili za wazi!