magnifico
JF-Expert Member
- Jan 14, 2013
- 11,075
- 24,634
Ndugu zetu Simba msimu huu wamekuja na kauli mbiu hizi, Yanga anabebwa, Yanga ananunua mechi, GSM anatuharibia ligi na kuna muda wakipagawa zaidi utawasikia wanasema Yanga imeshuka kiwango.
Maoni yangu, mafanikio ya Yanga yanaanzia kwenye uongozi. Sitaki kumuingiza GSM japo nae anaplay part kubwa tu. Lakini GSM ni nani mbele ya tajiri mkubwa Afrika Mo Dewji?
Simba na Yanga wote wana pesa kipindi hiki lakini mmoja ukimuangalia anazidi kusogea mbele kwa kasi huku mwingine akiwa na mwendo wa kusuasua. Hii maana yake kuna shida kwenye uongozi, kuna shida kwenye timu ya usajili.
Angalia replacements za wachezaji zinavyofanyika pale Yanga. Angalia wanavyopigania mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa timu. Je, mnaona dalili za hawa watu kupoteana kwa siku za karibuni hizi.
Ubaya wa kuhonga ili ushinde mechi lazima uumbuke ukienda kimataifa lakini kwa Yanga hali ni tofauti. Angalia matokeo yake kwenye michuano ya CAF.
Hizi kauli mbiu mlizokuja nazo msimu huu zitakuja kuwahukumu ninyi wenyewe.
Asili ya Mtanzania ni kufanya kazi vizuri na kwa ufanisi akiwa kwenye pressure. Bahati nzuri nyie wenzetu pressure mmeielekeza kwa Marefa, TFF na GSM huku mkiachana na uongozi wenu.
Mmeshawahi kujiuliza kwenye kikosi chenu cha Mabilioni nani anapenya kwenye first eleven ya Yanga? Kama ukiulizwa kati ya Ateba na Mzize nani aanze unapata kigugumizi vipi kwa hao wengine?
Kama mtaendelea kuwanyoshea vidole wengine mkaacha kujitathimini madhaifu yenu hapatakuwa na wakuizuia Yanga yenye uongozi imara.
Mo Dewji aweke mtu wa kulinda uwekezaji wake pale Simba kama alivyofanya kipindi kile cha Babra na kama anavyofanya GSM kipindi hiki. Inawezekana pesa anatoa kweli ila upigaji ni mwingi.