DITOPILE WAPILI
JF-Expert Member
- Oct 19, 2015
- 384
- 261
Klabu ya Simba itaendelea kuwa kichwa cha Mwendawazimu, kufungwa na kutofanya vizuri katika michuano ya Afrika iwapo itaendelea kushikiria akili na tamaduzi hizi,
Taarifa zinasambaa Papy Kambamba Tshishimbi anaondoka Yanga kuelekea Simba, taarifa hii imesambaa kwenye vyombo vya habari, pia post iliyotumwa na mchezaji wa SIMBA Ibrahimu Ajibu inaashiria Tshishimbi atatua SIMBA.
Kama kweli Simba inataka kufanya vizuri inabidi kuachana na wachezaji wa viwango vya kati, watafute mchezaji mkubwa kwa ajili ya kwenda kushinda mataji makubwa ya Afrika.
Tshimbimbi sio mchezaji mbaya, hapana, naheshimu uwezo wa mchezaji huyu lakini kwa sasa Simba haitaji mchezaji wa kiwango chake.
Timu inahitaji wachezaji kama watatu (3) wakubwa, wanao cheza ligi na mashindano makubwa sio wachezaji wa wakujaribu jaribu.
Timu inasajiri wachezaji kiushabiki halafu wanakuwa hawana msaada kwenye mashindano kwenye mashindano makubwa.

Kama hizi taarifa za Tshishimbi kusaini Simba ni kweli basi kwenye bodi ya Simba kuna tatizo kubwa sana. Ni muda mrefu sana Simba ilikuwa inaongoza ligi hivyo kuwa na uhakika wa kushiriki michezo ya kimataifa kwa sababu hiyo ilitakiwa mpaka sasa iwe tayari imeshamaliza usajili wake kitambo sana. Sasa tetesi hizi za usajili mara Morison mara Tshishimbi inaelekea tatizo la mwaka jana la usajili bado halijatafutiwa ufumbuzi. Tshishimbi namkubali sana kwenye ligi ya ndani lakini kutokana na umri wake, majeraha ya mara kwa mara na kiwango chake kupanda na kushuka mara kwa mara sidhani kama ni wakati sahihi sasa kwa Simba kumsajili. Iwapo Simba wangemsajili Tshishimbi miaka miwili mitatu iliyopita kweli ningewasifu kwani wakati ule jamaa alikuwa moto wa kuotea mbali.
Simba kwa sasa inahitajika kusajili wachezaji wakupambana kwenye ligi ya mabingwa Afrika.Kwa mtizamo wangu mimi sioni kama Tshishimbi atakwenda kuongeza kitu kipya Simba. Simba ni timu kubwa sana kusubiri mpaka Yanga wawafanyie "scouting" ya wachezaji ni aibu sana. Hivi siku zote huwa najiuliza wale viongozi wa zamani wa Simba waliowaleta akina Okwi, Mafisango, Joseph Owino, Pawasa, Emmanuel Gabriel, Mbwana Samata n.k. si bado wapo . Viongozi wa sasa wasione aibu waende tu wakawaulize walikuwa wanafanyaje kuwapata wachezaji stahiki wenye viwango vya kuchezea Simba kuliko kuanza kuokota mara Tshishimbi au kuanza kugombana na Yanga juu ya mchezaji wao mpya mwenye kiwango Morisson.
Hivi viongozi wa Simba wameshajiuliza kuwa kuna wakina Morisson na Luis wangapi ambao hawana namba za kudumu kwenye timu kubwa za Afrika Kusini tu achilia mbali timu nyingine kubwa za Afrika ambazo zinajua nini maana ya "scouting"?. Nendeni mkawakusanya hao vijana kama wanne au watano hivi nina hakika mtatengeneza timu tishio Afrika ndani ya miaka miwili/mitatu tu. Wachezaji waandamizi wenye umri mkubwa wapo wa kutosha Simba ni wakati sasa wa kusajili vijana wenye vipaji na kiu ya mafanikio na matokeo yataonekana ndani ya muda mfupi.