Simba wataendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu

DITOPILE WAPILI

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
384
Reaction score
261
Klabu ya Simba itaendelea kuwa kichwa cha Mwendawazimu, kufungwa na kutofanya vizuri katika michuano ya Afrika iwapo itaendelea kushikiria akili na tamaduzi hizi,

Taarifa zinasambaa Papy Kambamba Tshishimbi anaondoka Yanga kuelekea Simba, taarifa hii imesambaa kwenye vyombo vya habari, pia post iliyotumwa na mchezaji wa SIMBA Ibrahimu Ajibu inaashiria Tshishimbi atatua SIMBA.

Kama kweli Simba inataka kufanya vizuri inabidi kuachana na wachezaji wa viwango vya kati, watafute mchezaji mkubwa kwa ajili ya kwenda kushinda mataji makubwa ya Afrika.

Tshimbimbi sio mchezaji mbaya, hapana, naheshimu uwezo wa mchezaji huyu lakini kwa sasa Simba haitaji mchezaji wa kiwango chake.

Timu inahitaji wachezaji kama watatu (3) wakubwa, wanao cheza ligi na mashindano makubwa sio wachezaji wa wakujaribu jaribu.

Timu inasajiri wachezaji kiushabiki halafu wanakuwa hawana msaada kwenye mashindano kwenye mashindano makubwa.

"Tshimbimbi sio mchezaji mbaya, hapana naheshimu uwezo wa mchezaji huyu lakini kwa sasa Simba haitaji mchezaji wa kiwango chake'"

Simba ni timu kubwa, Tshimbimbi kabamba ni mchezaji mkubwa hapa kila upande naona utanufaika kama ni kweli
 
Simba ina rasilimali nyingi tu lakini wanashindwa kuzitumia mnazijaza stoo tu zipigwe na vumbi. Fraga mchezaji mzuri sana lakini wanamsugulisha benchi, Mlipili sijui kipi kawakosea Simba, Ajib na Gadier kwenye ubora wao Yanga, kwenda Simba wamekuwa wachezaji wa kawaida kabisa wanaozea benchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Tshimbimbi sio mchezaji mbaya, hapana naheshimu uwezo wa mchezaji huyu lakini kwa sasa Simba haitaji mchezaji wa kiwango chake'"

Simba ni timu kubwa, Tshimbimbi kabamba ni mchezaji mkubwa hapa kila upande naona utanufaika kama ni kweli
Kuna watu wanaona kama wengine hawatumii akili. Simba sio mtu ni taasisi tena vichwa. Wakidhani weo wanaweza kufikiria zaidi ya Board ya Simba wanajidanganya. Halafu hao wachezaji wakubwa unajua thamani zao? Wale sio kuku tu unaenda kuchukua sokoni. Kwa hiyo Simba inajua imchukue nani kwa ajili ya nini na kwa budget ipi.
 
Acha kutoa mapovu, Ukiona wanaenda kinyume na wewe nunua timu yako uendeshe unavyojua uwalete hao wachezaji wakubwa alafu acha maneno mbao inauzwa tena bei ya nyanya kabisa
 
Ya Simba waachie Simba mnatakiwa mujadili mkataba wenu na GSM. Kwanini mambo 8 waliyoyataja kwenye barua yao leo HAYAPO KWENYE MKATABA WENU.

Kwenye mkataba wenu mlikubaliana nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa ni kuwasusia tunawapa vichwa sana tunavyojaa uwanjani Tshishimbi au Yondani sio wa kiwango cha kucheza hii Simba kumbuka Uchebe alimkataa hata yule beki wao tegemeo Lamini Moro ingawa aliletewa magarasa mengine.
 
"Tshimbimbi sio mchezaji mbaya, hapana naheshimu uwezo wa mchezaji huyu lakini kwa sasa Simba haitaji mchezaji wa kiwango chake'"

Simba ni timu kubwa, Tshimbimbi kabamba ni mchezaji mkubwa hapa kila upande naona utanufaika kama ni kweli
Ni kweli tumchukue huyo Tshishimbi na pia Morrison.
 
simba ni bora kama ingemsajili fei toto mwenye umri mdogo na muda mrefu wa kukijenga kikosi cha simba kuliko kumsajili mzee shishimbi ambae anenda kuongeza matata kwenye kikosi
 
"Tshimbimbi sio mchezaji mbaya, hapana naheshimu uwezo wa mchezaji huyu lakini kwa sasa Simba haitaji mchezaji wa kiwango chake'"

Simba ni timu kubwa, Tshimbimbi kabamba ni mchezaji mkubwa hapa kila upande naona utanufaika kama ni kweli
kwa hatua ilipo Simba sasa hivi, Simba inaangalia zaidi mashindano ya Afrika ambayo Tshishimbi hana maajabu wala nafasi ya kuinufahisha Simba.

Tshimbimbi ni mchezaji mkubwa kwa ligi yetu na kombe la mapinduzi.
 
Unazungumzia ile bodi ambayo, inafanya kile anachotaka Mo?
 
dawa ni kuwasusia tunawapa vichwa sana tunavyojaa uwanjani Tshishimbi au Yondani sio wa kiwango cha kucheza hii Simba kumbuka Uchebe alimkataa hata yule beki wao tegemeo Lamini Moro ingawa aliletewa magarasa mengine
Kweli kabisa yaani pesa ya kununua wachezaji wa kawaida fungu zima, Bora kununua mchezaji mmoja au wawili lakini ni GOALS MACHINE halafu awe na umri mdogo.
 
naungana na wewe kwenye hili tatzo hatuna pakusemea sio muda tena wa kutafuta wacheyaji wa kati kama mnataka kufika mbali kimashindano za klab bingwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…