Simba watajisahau tena

Simba watajisahau tena

canfi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2022
Posts
1,368
Reaction score
1,477
Tangu mechi za ngao ya jamii hawakuonesha maajabu, lkn kwakuwa walichukua kombe (kwa penati za mazabe ya kipa wao) wakajisahau kuwa wana timu mbovu. Baada ya kuanza kwa kusuasua kwenye ligi ya mabingwa africa (kwa sare mfululizo) wakaanza manung'uniko ya timu mbovu na kocha hafai.

Muda mfupi baadae, Yanga akapigwa na Ihefu. Simba wakajisahau tena kuwa wana manung'uniko yao. Wakarudi mtaani kifua mbele kuwa wao ni bora sana (kwa kuwa tu Yanga kafungwa na Ihefu). Walipotandikwa 5-1 wakarejea kwenye manung'uniko yao hadi kumtimua kocha.

Wamebadili kocha lkn bado timu haijastawi. Haichezi vizuri na tayari wamedondosha points kwa KMC. Hata Mapinduzi cup hawajacheza vizuri. Lkn ikitokea wamechukua kombe la Mapinduzi, watajisahau tena (kama ilivyo kawaida yao). Wanasahau mambo ya msingi kwa vitu vidogo saaana. Hao ndio Simba
 
Hahaha pira la bongo liendelee watupe burudani😂😂
 
Ku Bebwa kwa Simba ni mtaji kwa Yanga kwakua inaficha madhaifu Yao mengi Hali itakayo saidia kuendelea kumfunga na ku twaa Mataji ya maana yakutosha.
 
Simba wanafuatiliwa zaidi na Yanga na manung'uniko hufanywa na Yanga kwa niaba yao.
 
Alikupiga hamsa huyo
Hivi nyie uto mbona hyo 5 mnajifanya kama hamjawahi fungwa???
Screenshot_20240110-182811_Instagram.jpg
 
Ku Bebwa kwa Simba ni mtaji kwa Yanga kwakua inaficha madhaifu Yao mengi Hali itakayo saidia kuendelea kumfunga na ku twaa Mataji ya maana yakitosha.
Upo sahihi.Natamani sana Simba atwae hili kombe.
 
Ulikua unasikiza kwenye redio au ulikua unautazama live tuanzie hapo
Maana naona mara dakika, mara kona mara kagere ila sijasikia mtu akitia neno baada ya beki wa Singida kunawa mpira ndani ya 18yard.
 
Back
Top Bottom