SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Mimi kwa kuwa ni mpenzi wa dhati wa soka, nimewahi kukaa na kuangalia mechi na wachezaji wa zamani na kujua kwa kina historia mbalimbali za soka maana bila kujua ulipotoka hauwezi kujua unapokwenda.
Leo nimewaza timu ya Simba inayoonekana kuwa na wakongwe wengi ambao wanaelekea ukingoni mwa career zao kama top players. Wakati mwingine hii inaongelewa kama ni udhaifu lakini kuwa na balance nzuri ya wachezaji wakongwe na vijana ni muhimu sana kwa championship team yoyote.
Mwaka 1990, timu ya taifa ya Cameroon, maarufu kama Indomitable Lions, ilikuwa ni nchi ya kwanza kutoka Afrika kuingia robo fainali katika Kombe la Dunia. Timu hiyo ilikuwa na wachezaji wengi wakongwe waliokuwa wanaenda kumaliza career zao na ilienda kuweka historia.
Walikuwa wanacheza mpira wa kuvutia, wenye madoido mengi, walikuwa na confidence ya hali ya juu hata walipokuwa wanacheza na miamba ya soka duniani. Ni aina ya timu ambazo zinatokea mara moja baada ya vizazi vingi kupita.
Naiona Simba hii ya wakongwe hawa kina Manula, Chama, Kapombe, Mzamiru na Onyango wakiwa wamechanyanyika na vijana kama Kanoute, Sakho na Banda.
Simba unaweza kusema wana character fulani ya timu inayojiamini, watakupa kila kitu ambacho The Indomitable Lions ya kina Roger Miller, Francois Omam Biyik, Mackanacky na wengine walikuwa wanakupa.
Kuna hadi magoli wanayofunga Simba yanafanana na magoli niliyoona walikuwa wanafunga Cameroon ya kipindi kile.
Embu ngoja tuone itakuwaje.