Misimu yote ambayo tulisajili na watu wakafurahi sana kiasi cha kuweka matarajio makubwa basi tuliangukia pua huko kimataifa.
Ule msimu tumesajili akina Shiboub Simba sc ilionekana tishio lakin tulitolewa na akina UD SONGO, haya huu wa mwaka jana tulileta rundo la wachezaji na kila mtu akafurahi lakini matokeo yake kila mtu anayajua baada ya kuondoshwa na akina Jwaneng na ligi kuu ndo ikawa hivyo.
Me mpaka sasa sijaona sehemu ambapo Simba Sc imekosea kusajili kutokana na maingizo yake mapya (kama yote yatatimia kama zilivyo tetesi), kwasababu sehemu pekee iliyofanya team yetu ionekane mbaya msimu uliopita imerekebishwa, namaanisha (ushambuliaji na kiungo).
Simba hakuwa mbaya kiasi hicho, kama jinsi mnavyotaka kuikuza, kufeli kwa simba Sc msimu uliopita ni kukosa washambuliaji wa kumalizia nafasi zilizotengenezwa.