Klabu ya Simba SC imegomea kampuni mpya iliyopitishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya uuzaji wa tiketi za mchezo wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga SC, unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 10, 2026.
Simba SC imechukua hatua hiyo kwa kuandika barua rasmi kwenda Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), ikipinga kampuni hiyo mpya iliyopitishwa na TFF kwa ajili ya kushughulikia uuzaji wa tiketi za mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.
Soma pia: Bodi ya Ligi kuweka ‘Gas Detector’ kukagua hewa Vyumba vya kubadilishia nguo Dabi ya Kariakoo
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitarajia kutumia
vendor mpya wa ukataji tiketi katika msimu wa 2026/2027, tofauti na aliyekuwa akitumika awali. Kuchelewa kwa zoezi la uuzaji tiketi za Dabi ya Kariakoo kunatajwa kuhusishwa na kutokuwepo kwa makubaliano kati ya Simba SC na Bodi ya Ligi (TPLB) kuhusu vendor huyo mpya, baada ya kikao kilichofanyika leo.
Katika kikao hicho, TPLB ilimtambulisha vendor mpya kwa Simba SC, lakini pande hizo hazikufikia makubaliano kutokana na
asilimia ya makato kwenye mapato ya mchezo. Vendor mpya anatarajiwa kukata asilimia 10 ya mapato ya jumla kabla ya kukatwa VAT ya asilimia 18, huku vendor aliyeondolewa alikuwa akichukua asilimia 16 kwa kila tiketi.
Hatua hiyo imekuja ikiwa zimesalia siku tatu pekee kabla ya Dabi ya Kariakoo, ambayo inatarajiwa kuwakutanisha watani hao wa jadi katika dimba la Uhuru (Shamba la Bibi) majira ya Saa !:00 Usiku.
Kabla ya msimu wa 2026/27, uuzaji wa tiketi za michezo ya Ligi Kuu ulihusisha zaidi
mfumo wa N-CARD, huku tiketi zikipatikana kupitia vituo maalum vya mauzo na pia mitandao ya simu.
Kanuni za Ligi zilizokuwa zikifanya kazi msimu huo pia ziliipa
klabu mwenyeji mamlaka ya kusimamia shughuli za maandalizi ya mchezo, ikiwemo
mchakato wa uuzaji wa tiketi kwa njia ya kielektroniki, huku TFF/TPLB ikiwa na jukumu la kutoa mwongozo wa uuzaji huo.
Nini kimebadilika msimu wa 2026/27?
Mabadiliko makubwa yamekuja kupitia marekebisho ya Kanuni za Ligi yaliyofanywa na TFF Julai 2026. Katika
kanuni hizo mpya,
TFF/TPLB ndiyo yenye jukumu la kusimamia na kuratibu mchakato wa kumpata
mzabuni/vendor wa
kuuza tiketi kwa mashindano yote yaliyo chini yake.
Mfumo mpya ulianza lini?
Mfumo mpya wa ununuzi wa tiketi ulianza kutumika msimu huu wa 2026/27, kuanzia
Simba Day, Yanga Day na Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga, iliyochezwa Agosti 12, 2026 Zanzibar.
TFF ilianzisha mfumo wa
kidijitali, unaowawezesha mashabiki kununua tiketi kwa njia ya mtandao bila kulazimika kufika vituoni, kama ambavyo video hapo chini inaonesha hatua za ununuzi wa Tiketi.