Simba yaingia mkataba na Equity Bank kwenye card za Uanachama Simba

ZionGate

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
6,362
Reaction score
2,991
Klabu ya Simba leo imeingia mkataba na benki ya Equity ambao utawezesha benki hiyo kusimamia mradi wa kadi mpya za wanachama na mashabiki ambazo zitaitwa Simba Card.

Kadi hizo zitatumiwa na wanachama na mashabiki kuweka akiba ye pesa na kutoa pindi wanapotaka kutumia, lakini pia kulipa ada ya kila mwaka, kununua tiketi za kuingia mpirani, na kupata punguzo la mpaka 10% kwenye maduka makubwa ambayo yatashirikiana na Simba

Faida kubwa kwa klabu katika kadi hizo ni makato yanayopatikana wakati wa kufungua akaunti, kukusanya ada kisasa na mara moja kwa mwaka, na kupata takwimu sahihi za mashabiki iwapo kila shabiki atafungua akaunti.

Kadi hizo zitaanza kutolewa Septemba mosi mwaka huu kwa kuwabadilishia kadi wanachama wa sasa na baadae zoezi litaendelea kwa wanachama wapya na mashabiki
 
Naona Simba wako kibiashara zaidi na jezi UHL itauza nyingi sana
 
UHL watarudisha hela za udhamini wa miaka 2 kwa kuuza jezi 20000 tu kwa 30000
 
m mwana simba ila napenda mtifuano kati ya mwanayanga na mwanasimba
 
Naona wale wazee. Wana ngangana na Hati na jengo huku mo akiendelea kujenga timu. Nawaambiatu wakina kilomoni hata wakitaka kuchukua jengo wachukuetu maana ndio fikra zao kwamba mo anataka jengo.
 
Wakuu hizi watangaze mapema sehemu ya kuipata,lazima nichangie simba,sh 14,500 kitu gani kwa mwaka wakati juhudi zinaonekana.

Simba ni timu yenye vision kwa sasa wengine wanafuata nyuma,ni matumaini yangu vilabu vingine vya Tanzania vitaiga vitu vizuri kupitia Simba.
 
Kwa taarifa yako suala la kadi jipya hata kidogo, ila kwa kuwa nninyi ni mbu x 3 mtaqashangilia kina Magori eti no wabunifu kumbe siyo, maana hadi sasa kuna wanachama tunazo kadi za benki ya posta. Na zinafanya kazi kama hizo zilizolezwa hapo juu. Hata wanachama wa Simba wanazo pia. Kwa hiyo hapo Magori kakopi na kupaste alichoanzisha mwenzake huko nyuma.
 
Bora uwatoe tongo tongo hawa kondoo wa Manara na Magori maana wao kazi yao kusema ndio tuu na kusifia
 
Leteni basi feedback hizo kadi kiasi gani mmechangia,au mmekaa nazo kama urembo
 
Mngekuwa na mfumo wa kadi unaoeleweka msingechangisha pesa kwenye vikapu.Wacheni kujikuza huku njaa kali.Juzi mlimuomba Andrew Vincent aendelee kucheza kwa mali kauli kwani klabu haina pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…