Simba yaitega Yanga

Simba yaitega Yanga

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
BASI%20LA%20SIMBA.jpg


Hata hivyo, Simba ambayo imeweka kambi Zanzibar kujiandaa na mchezo huo, itawasili Dar es Salaam Jumamosi saa 2:00 asubuhi na kuelekea moja kwa moja Hoteli ya Golden Tulip kupumzika kabla ya kutinga Uwanja wa Uhuru tayari kwa mchezo wao.

Akizungumza na Nipashe jana, Mratibu wa klabu hiyo, Abbas Ally, aliliambia Nipashe kuwa kwa sasa wachezaji wa timu hiyo wanaendelea na program yao kujiandaa na mchezo huo wa Jumamosi.

“Wachezaji wana morali ya juu, kila mmoja anauwaza na kuu kiria mchezo wa Juma- mosi..., kocha ( Joseph Omog) amekuwa akiwa- sisitizia umuhimu wa kushinda mchezo huu,” alisema Abbas.

“Hata kocha msaidizi (Masoud Djuma) ame- kuwa akiwahamasisha na amekuwa ra ki wa wachezaji kwa muda mfupi tu..., kiukweli kila kitu kinaenda sawa,” alisema Abbas.

Alisema mpaka ku kia jana, kikosi hicho cha wachezaji 24 kilichopo Zanzibar hakina maje- ruhi yoyote. “Leo ( jana) tumefanya mazoezi asubuhi na hatutakuwa na mazoezi ya jioni, ke- sho (leo) tunaendelea na mazoezi kwa kufuata program ya mwalimu,” alisema Abbas.

Simba inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesakama ilivyo kwa watani zao Yanga, imewaacha jijini Dar es Salaam wachezaji wake majeruhi Shomari Kapombe, Salim Mbonde pamoja na Said Mohamed ‘Nduda’ ambao wanaendelea kujiuguza.

Mchezo huo wa Jumamosi utatoa picha ya kinara katika msimamo wa ligi, kwa sasa Simba wanaongoza ligi kwa tofauti ya mabao huku ikigongana na Yanga kwa pointi, zote zina poin- ti 15 sawa na Mtibwa Sugar inayoshika nafasi ya tatu.

Hata hivyo, ushindani mkubwa upo kwa washambuliaji wa timu hizo, Emmanuel Okwi wa Simba na Ibrahim Ajibu wa Yanga ambao wamekuwa gumzo kwenye vikosi vyao huku wakifukuzana kwa mabao ya kufunga. Okwi ana mabao nane huku Ajibu akiwa na mabao matano .


IPP Media
 
Mechii hii hadi kipindi chakwanza kinaisha kunatimu itakua imeishapigwa 3-0
Tena rekodi yakibadeni inafikia ukingoni wakufunga goli 3 kwa mchezo wa watani
 
Sipati picha wakianza Ngoma,Ajibu ,Tambwe na Chirwa pale mbele..nafwaaaa
 
Tahadhali mashabiki wale wa kikosi cha bilion 1.3 msing'oe viti tu vya uwanjani na sebuleni mtakapokuwa mnaangalia mechi
 
Cross over players: Simba wanaye Niyonzima tu na Yanga wana Yondani, Tambwe, Ajibu, Kessy na yule wa almanusura Buswita. Sijui kama inamaana kwa game hii.
 
Badaam batamwagikaaaaa....... mtu lazima afe mapemaaa
 
Yanga hapa hatoki labda wajilinde wasifungwe. Kwa mechi hii msifikiri ni simba ile yaku droo na mbao. Hapa yanga mtakutana na timu nyingine kabisa kimchezo.
 
dk 90 zinaisha mpira umemalizika na simba wapo juu kwa ushindi.

itunze hii coment kesho mpira ukiisha utai-like fasta.
 
Back
Top Bottom