Simba yajitoa Kagame Cup

Konaball

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
2,949
Reaction score
1,940
Klabu ya Simba SC imepanga kujitoa kwenye michuano ya Kagame Cup yanayotarajia kufanyika July 07 hadi July 21 nchini Rwanda. Ceo wa klabu hiyo Crescentus Magori amesema watapeleka barua rasmi kwenye Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuwajulisha kutoshiriki mashindano hayo kwa sababu za kiufundi.
.
Magori amesema iwapo watashiriki mashindano hayo hawatapata muda wa kuweka kambi nje ya nchi kwa sababu mashindano hayo yanaisha July 21 na mashindano ya Afrika Caf Champions League raundi ya awali yataanza August 9-11 mechi za mkondo wa kwanza na August 23-25 mechi za mkondo wa pili na ligi kuu Tanzania Bara itaanza mwishoni mwa mwezi wa nane (August)
.
Mechi za raundi ya Kwanza za Caf Champions League zitaanza September 13-15 na mechi za mkondo wa pili raundi ya kwanza zitachezwa September 27-29. Magori amedai kutokana na sababu za kubadilika kwa ratiba ya CAF, michuano ya Afcon yatakayofanyika Misri itakuwa ngumu kwa klabu ya Simba kushiriki mashindano ya Kagame Cup. Simba inatarajia kwenda kuweka kambi ya mwezi mmoja nje ya nchi kujiandaa na msimu wa 2019/20.
 
Naunga mkono hoja, viongozi msikubali hili bonanza likatupotezea muda wa kuaandaa timu yetu Kwa ajili kwenda kunyakua kombe la club bingwa Afrika.

Wakigombaa Sana maana bila Simba mashindano hayanogi basi wapelekeni Simba queen, hao chura wakachakazwa na Simba queen mpaka wachakaee!

Wakigomaa pelekeni under17.

Tuko bize kuiwakilisha na kuiletea nchi heshima eboo!
 

Nyie si ndio mlikuwa mnajivunia kuwa ndio mabingwa wa kihistoria wa hilo Kombe, sasa hivi limekuwa kombe la mbuzi
 
Naunga mkono hoja pia ikibidi na mapinduzi cup waipotezee
 
wachezaji wa simba wamechoka sana na wengine watakuwa wanatoka misri ,bora hizo 6 weeks zikatumike kambini kutengeneza muunganiko na kuzoeana mapema, vvyura nendeni mkachukue hilo kombe
 
Maneno meeengi, lkn sababu kubwa ni kujumuishwa kwa Yanga kwenye mashindano hayo. Lzm waogope
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…