Klabu ya Simba SC imepanga kujitoa kwenye michuano ya Kagame Cup yanayotarajia kufanyika July 07 hadi July 21 nchini Rwanda. Ceo wa klabu hiyo Crescentus Magori amesema watapeleka barua rasmi kwenye Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuwajulisha kutoshiriki mashindano hayo kwa sababu za kiufundi.
.
Magori amesema iwapo watashiriki mashindano hayo hawatapata muda wa kuweka kambi nje ya nchi kwa sababu mashindano hayo yanaisha July 21 na mashindano ya Afrika Caf Champions League raundi ya awali yataanza August 9-11 mechi za mkondo wa kwanza na August 23-25 mechi za mkondo wa pili na ligi kuu Tanzania Bara itaanza mwishoni mwa mwezi wa nane (August)
.
Mechi za raundi ya Kwanza za Caf Champions League zitaanza September 13-15 na mechi za mkondo wa pili raundi ya kwanza zitachezwa September 27-29. Magori amedai kutokana na sababu za kubadilika kwa ratiba ya CAF, michuano ya Afcon yatakayofanyika Misri itakuwa ngumu kwa klabu ya Simba kushiriki mashindano ya Kagame Cup. Simba inatarajia kwenda kuweka kambi ya mwezi mmoja nje ya nchi kujiandaa na msimu wa 2019/20.