Simba yakanusha uzushi wa mitandaoni kuhusu kuondolewa kwa kocha na benchi la ufundi

Simba yakanusha uzushi wa mitandaoni kuhusu kuondolewa kwa kocha na benchi la ufundi

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
SIMBA YAKANUSHA UVUMI WA KUMFUKUZA KOCHA OMOG

Klabu ya Simba haijatoa taarifa yeyote kuhusiana na mabadiliko yanayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasioitakia mema klabu yetu.

‘Nimeshaeleza toka awali kuwa, hakuna mechi tano wala huo mpango wa kumwondoa kocha Omog au benchi zima la ufundi, klabu ya Simba haina mpango huo.

'Tunaomba mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba kuweka Imani yao kwa Uongozi, kikosi cha Simba na benchi la ufundi kuwa tunajua nini mashabiki wetu wanachotaka na ndicho tunachopambana kuhakikisha tunafikia malengo' alisema Haji Manara alipoongea na Simba News kuhusiana na ujumbe unaosambazwa wa kuvunjwa kwa benchi la ufundi la Simba.

Klabu ya Simba itaendelea kuhakikisha inatoa taarifa sahihi na kwa wakati kupitia njia zake za mawasiliano chini ya Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Haji Manara na sio kwingineko
 
Hivi sijui na nyie wenzangu mmekigundua hiki kitu. Timu za Tanzania zinapoanza kufanya vizuri tu lazima wavuruge waanze upya. Rejea Yanga ya Pluijm na ushiriki wake wa Kimataifa, Rejea Simba ya Patric Phiri, Rejea Majimaji ya Kally Ongala, Rejea Mbeya City ya Mwambusi, Rejea Azam ya Stuart Hall, Rejea Taifa Stars ya Kim Poulsen na muda sio mrefu tutarejea Simba ya Omog.
 
Mashabiki WA simba na yanga ni wapumbavu daima ni wachovu WA akili na hekima hawajui mpira wanajua majungu na fitina wanaangalia mpira WA ulaya lkn hawajifunzi wenzetu walivyo wavumilivu na wastarabu.. Timu imecheza mechi 4 haijafungwa eti Mnataka kocha afukuzwa ni ujinga huo. Kocha mpya akija lini atatengeneza timu isifungwa ligi ikiwa inaendelea.
 
SIMBA YAKANUSHA UVUMI WA KUMFUKUZA KOCHA OMOG

Klabu ya Simba haijatoa taarifa yeyote kuhusiana na mabadiliko yanayoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na watu wasioitakia mema klabu yetu.

‘Nimeshaeleza toka awali kuwa, hakuna mechi tano wala huo mpango wa kumwondoa kocha Omog au benchi zima la ufundi, klabu ya Simba haina mpango huo.

'Tunaomba mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Simba kuweka Imani yao kwa Uongozi, kikosi cha Simba na benchi la ufundi kuwa tunajua nini mashabiki wetu wanachotaka na ndicho tunachopambana kuhakikisha tunafikia malengo' alisema Haji Manara alipoongea na Simba News kuhusiana na ujumbe unaosambazwa wa kuvunjwa kwa benchi la ufundi la Simba.

Klabu ya Simba itaendelea kuhakikisha inatoa taarifa sahihi na kwa wakati kupitia njia zake za mawasiliano chini ya Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano Haji Manara na sio kwingineko
Lisemwalo lipo, na kama halipo, laja. Take note, halafu tutarudi tena hapahapa
 
Mashabiki WA simba na yanga ni wapumbavu daima ni wachovu WA akili na hekima hawajui mpira wanajua majungu na fitina wanaangalia mpira WA ulaya lkn hawajifunzi wenzetu walivyo wavumilivu na wastarabu.. Timu imecheza mechi 4 haijafungwa eti Mnataka kocha afukuzwa ni ujinga huo. Kocha mpya akija lini atatengeneza timu isifungwa ligi ikiwa inaendelea. Hakika mashabiki WA simba na yanga ni mazwazwa wajinga mtozeni
Na wewe ukiwemo mkuu.
 
Wamtimue tu si walimsajilia wao sasa kila shabiki anataka kumuona mchezaji wake dimbani kocha m bovu amefungwa mechi ngapi??
 
Back
Top Bottom