Simba yakataa kucheza na Yanga, kisa ni waamuzi. Yataka waamuzi wa nje

Queen V

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2012
Posts
775
Reaction score
1,332


Uongozi wa Klabu ya Simba, umetamka wazi kuwa, hautakuwa tayari timu yao kucheza mechi yoyote dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga huku waamuzi wakiwa ni Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara wakati akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo, Kariakoo jijini Dar.

Manara alisema sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kutokana na kila wanapokutana na Yanga kuonewa kwa makusudi na waamuzi ambao wanaonesha dhahiri kwamba wametumwa, hivyo wamechoka kuonewa, sasa wanataka haki itendeke kwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka nje.

“Tumecheza na Yanga mara nyingi tu, na mchezo wetu wa mwisho wa ligi kuu tulitoka sare ya bao 1-1, lakini mwamuzi wa kati siku ile, Martin Saanya alionekana dhahiri kutunyonga.

“Matukio ni mengi ya kustaajabisha yalitokea ikiwemo kulikataa bao letu halali na kulikubali la Yanga ambalo mfungaji kabla ya kufunga, aliukumbatia mpira kama mtoto, kisha akafunga, halafu mwamuzi eti anaita kati kuashiria bao.

“Haitoshi, wachezaji wetu wanalalamika, anakuja kumuadhibu nahodha wetu, Jonas Mkude kwa kumpa kadi nyekundu ya moja kwa moja, lakini kwa kuwa Mungu hamtupi mja wake, ile kadi ikaja kufutwa na Kamati ya Saa 72 ambayo iliona mwamuzi wao kachemsha.

“Kwa hali hii, hatutakuwa radhi kuingiza timu uwanjani endapo tu waamuzi wakiwa ni walewale. Tumechoka kuonewa,” alisema Manara.

Katika kukazia hilo, Manara alisema wapo radhi wao kama Simba, mapato yote ya mchezo wao dhidi ya Yanga wagharamie kila kitu kwa waamuzi hao wa nje ili waje wasimamie haki.

“Tutagharamia kila kitu kwa ajili ya waamuzi kutoka nje, hata mapato yetu yote ya mchezo tutatoa kwani tunataka haki itendeke, mbona nchi za wenzetu kama Misri wao wanaweza kufanya hivyo kwa mechi kubwa kama yetu hii, kwa nini sisi tushindwe,” alisema.

Aidha Manara alisema kutokana na Simba kuonewa mara kwa mara, kamati ya utendaji ya klabu hiyo, imefikia makubaliano ya kumuandikia barua Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TF), Jamal Malinzi ili wakutane waongee ni kwa nini klabu yao imekuwa ikionewa kila kukicha.

“Tumemwandikia barua Malinzi ya kumtaka tukae tuzungumze tuone Simba ina tatizo gani mpaka iwe inaonewa kila siku, tunataka tulifahamu hilo ili kuondoa hali hii ambayo sasa imetuchosha,” alisema Manara na kuongeza.

“Tumeitisha mkutano wetu wa wanachama kwa ajili ya mabadiliko ya katiba, halafu tunasikia kuna mtu huyu anajiita Mohammed Kiganja (Katibu wa BMT) eti anasema kitakachoafikiwa siku hiyo wao hawakitambui wakati waziri mwenyewe amekubali.

“Sasa huyu Kiganja ni nani hasa mpaka atuendeshe kiasi hiki, sisi tunasema, katika hili hakuna wa kutuzuia, tutafanya mabadiliko ya katiba kama wanachama wakikubali, hakuna wa kutuingia katika katiba yetu hata kama serikali ilihali hatuvunji katiba ya nchi.

“Hivi kwa soka la sasa ni nani asiyependa mabadiliko, huyu Kiganja yeye amekuwa akijitokeza kwenye migogoro tu, kwa nini katika maendeleo hayupo, tumefuata sheria zote za kuitisha mkutano na tutaufanya bila ya kizuizi chochote kile,” alimaliza Manara.


Chanzo: Salehe Jembe
 
Bora wagome watupunguzie homa ya mechi ya watani wa jadi
 
Tunaambiwa mpira ni wa tff nchi hii sio wa simba wala yangu haya majigambo yanatoka wapi.
 
Ukisikia kuishiwa au kutafuta sababu mapema ndiyo huku. Mwamuzi atoke nje harafu wamgharamie wao. Hiyo sio rushwa kwa hao waamuzi toka nje?
Akija anambiwa gharama zako zimelipwa na Simba. Huo sasa utani. Ingekuwa initiative ya TFF yenyewe afadhali. Lakini itakuwa a vote of no confidence kwa waamuzi wetu wenyewe.
Harafu tutegemee nani atawaamini waamuzi wetu ?
Siku walipoifunga Yanga goli tano mbona timu ya Yanga haikusema haina imani na waamuzi wetu.
Sasa hivi wanajenga chuki na waamuzi wetu na hili litawagharimu.
Rage hakukosea kuwaita mbumbumbu!
Mechi za Ndanda, Mtibwa zitachezeshwa na waamuzi toka sayari ipi? Au hawahawa wasiofaa kwa mechi dhidi ya Yanga?
Ni vyema Simba ikaomba kucheza ligi nchi nyingine kama Bongo wanaonewa sana.
 
Hahhaha mbumbumbu waoga haooooo
Wameanza kujenga mazingira ya kupokea kipigo ili wasingizie waamuzi. TFF iwamulike viongozi wa Simba. Kauli hizi zinachochea kung'oa viti wakifungwa.
Four years and still counting matopeni imewalevya
 
Mnegoma na kutumia viwanja vya ndani mkacheze Nje huko...makosa wanafanya waamuzi wote hata wa Nje au manara unaangalia mechi ya simba na yanga tu basi.
..
 
Kati ya zile tano tatu za penati lkn Yanga hawakuongea, mikia kusikia Lwandamila wameanza kuweweseka,mtulie kipigo kiko palepale
 
hivi huyu katibu wa BMT wanataka simba na yanga wafate taratibu gan mkutano mkuu si ndio unaofanya mabadiliko ya katiba anataka mkutano upi sasa
 
Tatizo sio waamuzi, bali wanataka waruhusiwe kung'oa viti.😀😀 wanasingizia tu waamuzi, janja ya nyani.
 
Mechi za simba na yanga, simba na prisons pamoja na simba na African Lyon zichezeshwe na waamuzi toka South Africa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…