Simba yakataa kucheza na Yanga, kisa ni waamuzi. Yataka waamuzi wa nje

Simba yakataa kucheza na Yanga, kisa ni waamuzi. Yataka waamuzi wa nje

Ndio kabisa... tumechoka na magoli yao ya mikono kutoka kwa mkodisho FC
 
Mechi za simba na yanga, simba na prisons pamoja na simba na African Lyon zichezeshwe na waamuzi toka South Africa
Acha nawewe kuquote habari ndefu unachosha wanaotumia simu,we vipi..Kuhusu Simba wawe na msimamo kabisa maana tumechoka kuonewa na marefa wa Mal inzi.Wawe na meno ila kutishia kugomea mechi itawagharimu kwa kweli.Ila kila mwenye ufahamu anaona tunaonewa,hasa kwa siku za karibuni
 
Ukitaka kuchezeshwa na marefa wa nje kuwa bingwa watakuja hao marefa wa nje
 
Simba wana hoja ya msingi! Kwann TFF hawataki waamuzi bora kutoka sehemu yoyote duniani wachezeshe mechi za Simba na Yanga?

Ni dhahiri kuwa waamuzi wengi wa ndani wamezishindwa hizi mechi kwa kuwa zimeonekana kuwa kubwa kuliko uwezo wao au mahaba binafsi lkn kubwa zaidi inaweza kuwa rushwa. Hatuhitaji kuona aina ya uvunjifu wa amani kama wa October 1.
 
HIVI HUYU HAJI MANARA ANA ELIMU GANI?
MAGUFULI AKIACHA KUWATEUA, MANENO KIBAOO!! KUMBE IQ ISSUE!!
Hajui ligi ni zaidi ya Simba na Yanga?

HAFAHAMU KUWA REFA KUTOKA NJE YA NCHI NDIO RAHISI KUNULIKA KULIKO WA NDANI? HUYU HAWAJIBISHWI NA TFF.
PIA SHERIA ZA FIFA HAZITAMBUI LIGI YA NDANI YA NCHI KUCHEZESHWA NA REFA WA NCHI NYINGINE.

HII MBEGE ALIYO KUNYWA HUYU JAMAA INA MMALIZA IQ.
 
Mvua zimenyesha bwawa la samaki huko jangwani linakwenda na maji. Msaada wa mafuriko unahitajika sana.Vyura ndio usiseme mpaka barabarani.
 
Hamna lolote hao wameona timu yao kwa sasa ni mbovu haina uwezo wa kucheza na yanga, simba inatakiwa wajitathmini upya kuanzia management yao hadi technical bench kuna mahali huwa wanakosea kila mwaka wanaishia kulalamika kama suruhisho ni kumpa timu MO wakubaliane na wampe kuliko kutoa visingizio vya kuonewa na Malinzi
 
Najua Yanga kwa vile wamelewa na kubebwa ... wapo tayari simba isitokee uwanjani .
Na simba bora kugoma , mechi ya goli la mkono ilidhihirisha yeboyebo wanabebwa.
 
Huyo manara aache upumbavu inamaana huwa wanaonewa kwenye mechi za yanga pekee? kama kuna mechi nyingine pia huwa wanaonewa kwanini asiombe waamuzi wote wa ligi watoke nje ya nchi? Tatizo pale msimbazi uongozi umeajiri watu wa majungu kuanzia katibu mkuu hadi huyo msemaji. Binafsi ni mshabiki wa villa squad msijesema ni waupande ule kutokana na maoni yangu.
 
View attachment 438465

Uongozi wa Klabu ya Simba, umetamka wazi kuwa, hautakuwa tayari timu yao kucheza mechi yoyote dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga huku waamuzi wakiwa ni Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara wakati akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo, Kariakoo jijini Dar.

Manara alisema sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kutokana na kila wanapokutana na Yanga kuonewa kwa makusudi na waamuzi ambao wanaonesha dhahiri kwamba wametumwa, hivyo wamechoka kuonewa, sasa wanataka haki itendeke kwa kuchezeshwa na waamuzi kutoka nje.

“Tumecheza na Yanga mara nyingi tu, na mchezo wetu wa mwisho wa ligi kuu tulitoka sare ya bao 1-1, lakini mwamuzi wa kati siku ile, Martin Saanya alionekana dhahiri kutunyonga.

“Matukio ni mengi ya kustaajabisha yalitokea ikiwemo kulikataa bao letu halali na kulikubali la Yanga ambalo mfungaji kabla ya kufunga, aliukumbatia mpira kama mtoto, kisha akafunga, halafu mwamuzi eti anaita kati kuashiria bao.

“Haitoshi, wachezaji wetu wanalalamika, anakuja kumuadhibu nahodha wetu, Jonas Mkude kwa kumpa kadi nyekundu ya moja kwa moja, lakini kwa kuwa Mungu hamtupi mja wake, ile kadi ikaja kufutwa na Kamati ya Saa 72 ambayo iliona mwamuzi wao kachemsha.

“Kwa hali hii, hatutakuwa radhi kuingiza timu uwanjani endapo tu waamuzi wakiwa ni walewale. Tumechoka kuonewa,” alisema Manara.

Katika kukazia hilo, Manara alisema wapo radhi wao kama Simba, mapato yote ya mchezo wao dhidi ya Yanga wagharamie kila kitu kwa waamuzi hao wa nje ili waje wasimamie haki.

“Tutagharamia kila kitu kwa ajili ya waamuzi kutoka nje, hata mapato yetu yote ya mchezo tutatoa kwani tunataka haki itendeke, mbona nchi za wenzetu kama Misri wao wanaweza kufanya hivyo kwa mechi kubwa kama yetu hii, kwa nini sisi tushindwe,” alisema.

Aidha Manara alisema kutokana na Simba kuonewa mara kwa mara, kamati ya utendaji ya klabu hiyo, imefikia makubaliano ya kumuandikia barua Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TF), Jamal Malinzi ili wakutane waongee ni kwa nini klabu yao imekuwa ikionewa kila kukicha.

“Tumemwandikia barua Malinzi ya kumtaka tukae tuzungumze tuone Simba ina tatizo gani mpaka iwe inaonewa kila siku, tunataka tulifahamu hilo ili kuondoa hali hii ambayo sasa imetuchosha,” alisema Manara na kuongeza.

“Tumeitisha mkutano wetu wa wanachama kwa ajili ya mabadiliko ya katiba, halafu tunasikia kuna mtu huyu anajiita Mohammed Kiganja (Katibu wa BMT) eti anasema kitakachoafikiwa siku hiyo wao hawakitambui wakati waziri mwenyewe amekubali.

“Sasa huyu Kiganja ni nani hasa mpaka atuendeshe kiasi hiki, sisi tunasema, katika hili hakuna wa kutuzuia, tutafanya mabadiliko ya katiba kama wanachama wakikubali, hakuna wa kutuingia katika katiba yetu hata kama serikali ilihali hatuvunji katiba ya nchi.

“Hivi kwa soka la sasa ni nani asiyependa mabadiliko, huyu Kiganja yeye amekuwa akijitokeza kwenye migogoro tu, kwa nini katika maendeleo hayupo, tumefuata sheria zote za kuitisha mkutano na tutaufanya bila ya kizuizi chochote kile,” alimaliza Manara.


Chanzo: Salehe Jembe
Kila siku watu mnalalamika na mitimu mibovu mara simva ooo yanga; azamu, hamna kaz za kufanya, hakuna mchezaji wala timu nzuri tanzania, mbona hao mnaowasifia wakikutanishwa pamoja timu ya taifa inakula za uso, kuna uzuri gani hapo, achen kutuandikia upumbavu humu mnashusha hadhi zenu
 
manara wewe ni mbu mbu mbu. tanzania itakuwa ya kwanza duniani kuazima marefa eti kisa kuogopa hujuma. vere fakeni
 
Swali la mtu ambaye hajawahi angalia mpira tangu kuzaliwa kama mimi. Hivi timu za ndani ya nchi zinaruhusiwa kuwa na refa toka nje? Wakikodi refa inabidi aje na washika vibendera wake nao hao watoke nchi tofauti ili wasipange matokeo. Sasa kwa hali ya sasa ya Whatsup, skype, fb kweli Simba itaweza? Mchukue refa toka Dodoma anaitwa Mnyora Chief yule ni kiboko wa wizi. Mwanamke wa shoka atachezesha na hakuna uongo. Chukua marefa wanawake tuu Simba. Ila mimi wakati nipo hai nilishabikia Yanga.
 
Back
Top Bottom