Simba yalaani matumizi ya Polisi kuwazuia kufanya mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba kuelekea mchezo wa dhidi ya Pamba

Simba yalaani matumizi ya Polisi kuwazuia kufanya mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba kuelekea mchezo wa dhidi ya Pamba

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
1732216737935.jpg

1732216743835.jpg

Soma pia: Vurugu kali zimezuka Uwanja wa CCM Kirumba wakati Simba SC ikifanya mazoezi kuelekea mechi na Pamba Jiji hapo kesho'

========
Uongozi wa klabu ya Simba umesikitishwa na vitendo visivyo vya kiungwana vilivyofanywa na viongozi wa timu ya Pamba Jiji FC, kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda kwa kutumia Askari Polisi mkoani humo.

Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu ya NBC, Simba tulipaswa kutumia Uwanja wa CCM Kirumba kufanya mazozezi ya mwisho kuelekea mchezo wetu wa kesho Novemba 22, dhidi ya Pamba lakini hali isiyokuwa ya kawaida maafisa wa timu hiyo waligoma kutoka Uwanjani.

Pamoja na jitihada zote za kuwasihi, kupisha mazoezi lakini viongozi wa Pamba hawakukubali na kuendelea kusalia Uwanjani wakijifungia katika chumba cha mikutano.

Muda mfupi baadae mazoezi yakiwa yanaendelea, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa, Mtanda akiambatana na maafisa wa Polisi waliokuwa na vyeo mbalimbali huku wengine wakiwa na silaha walifika uwanjani hapo na kuingia ndani ya uwanja bila maelezo ya msingi wanakwenda kufanya nini.

Baada ya timu kumaliza mazoezi na kutaka kuondoka uwanjani, gari ya Polisi lilizuia msafara wa wachezaji na makocha huku wakiwakamata na kuwapandisha kwenye gari lao Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu na Kocha Msaidizi, Selemani Matola ambao waliwaachia baada ya mabishano.

Simba tunalaani matumizi ya nguvu yaliyotumika katika sakata hili na kuwakamata maafisa wa klabu yetu bila ya sababu za msingi kwani jambo hilo linaonekana kama jitihada za kudhoofisha timu yetu kuelekea mchezo wa kesho.

Baadae Rweyemamu na Matola waliachiwa na msafara kurejea hotelini.

Simba tunalaani vitendo vya matumizi ya dola katika mpira wa miguu, na tunawakumbusha viongozi wenye Mamlaka kutumia mamlaka yao katika njia sahihi.

Imetolewa na

Idara ya Habari na Mawasiliano

Simba Sports Club

21, Novemba 2024.
 
Mheshimiwa Mtamda RC Mwanza Leo umefanya tukio la hovyo ambalo linaweza kukugharimu kama sio kukushushia heshima !
Kitendo çha kwenda uwanjani kushiriki kwenye fujo kati ya Viongozi wapsmbe wa Pamba ,ns Timu ya Simba ni natumizi mabaya ya madaraka yako ya Ukuu wa Mkoa!
Ukiwa kiongozi unatakiwa upunguze mihemko yaushabiki soka!
Pole sana kwa yatakayo kukkuta!
Halafu ile press uliyotos ndio itskayo kumaliza!
Press hiyo imeandikwa kitoto!
 
Nalaani kitendo cha huyo mkuu wa mkoa saidi mtanda kuivamia simba ikiwa inafanya mazoezi huo ni uhuni na huyo mkuu wa mkoa ni muhuni na mvuta bangi na wavuta bangi kama hawa sijui wanateuliwaje.
 
Sina maneno mengi lakini najiuliza maswali machache tu kuhusiana na kitendo cha RC wa Mwanza kuenda na polisi wengine wakiwa na silaha kwenye mazoezi ya Simba yeye akisema kuwa amekwenda kuzuia taharuki inayoweza kusababishwa na polisi aliowatuma yeye mwenyewe!
Mchezo wa soka una kanuni zake,waliovunja kanuni,wanapiga simu kuomba msaada wa kipolisi kwa mkuu wa mkoa?!! OCD hakuwepo? Hilo eneo halina mkuu wa wilaya?
Simba ndio wanawafanyia fujo pamba kwa lipi walilo nalo?
Kama RC alithubutu kufanya hivyo,ni wazi kuwa ni kwa vile Rais ni mama na nionavyo ni kwa vile anamdharau.
Iwapo Rais angekuwa mwanaume,RC hawezi kufanya maamuzi ya kitoto kama vile kwani yeye ni mtu mkubwa sana.Ana watu wengi wa kutuma lakini kwa sababu ya ukereketwa wa timu,akaamua kutumia mamlaka yake kuonyesha ubabe wake.

Iwapo Rais anaweza kuishi na viongozi wa namna hii,bila shaka nitakubaliana na wale wanaomuona kama dhaifu.Sidhani kama RC wa Mwanza anastahili kuwa pale.Mwanza inahitaji mtu mbunifu maana tangu yule RC mmaasai,Mwanza haijawahi kuwa na Mkuu wa Mkoa bora hadi leo
 
Back
Top Bottom