Simba yalamba donge nono

Simba yalamba donge nono

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za wachezaji imesema haioni haja ya kuendelea kumfungia kiungo aliyesaini kandarasi katika vilabu viwili tofauti ambaye ni Pius Buswita baada ya yeye kukubali kuilipa Simba Milioni 10.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Elias Mwanjala leo baada ya vilabu hivyo kukaa pamoja na kufikiana muafaka juu ya mchezo huyo.

"Vilabu vya Simba na Yanga vimeshakaa na kuongea ambapo wamekubaliana mchezaji huyo arudishie pesa aliyoichukua ili aweze kufunguliwa lakini tumpe onyo kali ili suala hili lisiweze kujitokeza kwa mara nyingine", amesema Mwanjala.

Hata hivyo, Kamati ya hiyo imesema lengo hasa la kuridhia kumtoa kifungoni Pius ni kutokana na kuona mpira ndiyo ajira yake ambayo anaitegemea.

Kwa upande mwingine, Klabu ya Simba wamedai walipwe pesa ya nauli ya ndege waliyomlipia mchezaji huyo pindi wamemchukua ambapo Yanga wamekubali kuilipa pesa hiyo.
 
Yanga hatunaga tabu na pesa ndogo kama hizo kwani nini!!
 
Ukiwa na sheria na taratibu zinazoweza kupindishwa kwa vijisababu mbalimbali bila kujali uzito wa hoja hatuwezi kukomesha baadhi ya tabia.
Vipi Simba kama wangekataa hela kwa madai kuwa wanahitaji huduma ya mchezaji huyo na yupo kwenye mipango ya kocha na klabu?
 
Mkuu, kama tungekomaa, msimu mzima Buswita alikua anaozea benchi. Ila kwakua Simba SC hatuna makuu, acha kijana akajaribu kuokoa Jahazi ambalo linazama.
 
hahhaha eti jahazi linazama, miaka ya karibuni simba huwa anaanza kwa mbwembwe ligi ikichanganya anakimbilia uswisi
 
Mkuu Sembo nafahamu muda wako wa kuwa eneo korofi kwasasa haujafika,nakutabiria ikifika Mwezi April Mwakani Simu yako itakata network.

Hahaha.. Mkuu, kwa Simba hii eneo korofi nikafanye nini?
 
Ukiwa na sheria na taratibu zinazoweza kupindishwa kwa vijisababu mbalimbali bila kujali uzito wa hoja hatuwezi kukomesha baadhi ya tabia.
Vipi Simba kama wangekataa hela kwa madai kuwa wanahitaji huduma ya mchezaji huyo na yupo kwenye mipango ya kocha na klabu?
Angekuwa Malinzi kwenye nafasi ya urais ungesikia kuwa malinzi anawapendelea yanga. kwa kuwa kuna mwanachama wa simba kwenye ile nafasi basi inaoneana sawa tu.
 
Kikuku fc waishukuru simba lasivyo tungewakalisha na uyo mchezaji toka mpodo fc
 
Angekuwa Malinzi kwenye nafasi ya urais ungesikia kuwa malinzi anawapendelea yanga. kwa kuwa kuna mwanachama wa simba kwenye ile nafasi basi inaoneana sawa tu.

Ndio maana tunazunguka hapa hapa.
 
Kuna mambo ya kujiuliza katika hili tusitoe hukumu tu.

TFF washukuriwe saana na Simba kwa kupindisha sheria ili tu BUSWITA AWEZE KUREJESHA FEDHA.

Yanga waliwazidi Simba baada ya kuwasiliana na Mbao ambao walimuachia BUSWITA kwenda Yanga kwa njia ya TMS Simba walipojaribu wakakwama.

Mkataba wa Simba na mchezaji si usajili kwani usajili unafanywa kwa TMS huu ni mfumo usioongopa wala kughushiwa hivyo ilikuwa njia pekee ni Simba kutafuta haki ya kurudishiwa pesa zao kupitia njia zingine za kisheria.

Ndo maana SIMBA hawakuweka pingamizi kwenye usajili wa BUSWITA, vile vile ndo maana Simba hawakupeleka TFF jina la BUSWITA na ndio maana msemaji wa Simba alisema Simba itampeleka BUSWITA mahakamani.

Ilichofanya TFF ni kuisaidia Simba kupata fedha zake kwa njia HARAMU ya kumfungia binafsi nilijua watamwachia tuu.
 
Kwa upande mwingine, Klabu ya Simba wamedai walipwe pesa ya nauli ya ndege waliyomlipia mchezaji huyo pindi wamemchukua ambapo Yanga wamekubali kuilipa pesa hiyo.

Yanga hatunaga tabu na pesa ndogo kama hizo kwani nini!!
pesa za poda hizoo
 
Mkuu, kama tungekomaa, msimu mzima Buswita alikua anaozea benchi. Ila kwakua Simba SC hatuna makuu, acha kijana akajaribu kuokoa Jahazi ambalo linazama.
Hahaha. Mkuu toa ya moyoni achani utani.
 
Back
Top Bottom