SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kutokana na propaganda zilizoenezwa na zilizodumu msimu mzima, ni rahisi sana kuamini Simba wamekuwa timu ya hovyo na rekodi ya hovyo sana msimu huu.
Nilishawahi kuleta uzi nikikumbushia Simba ndiyo timu iliyofungwa mechi chache msimu huu kuliko zote (mechi moja tu) na hadi msimu unamalizika leo hii bado ameshikilia rekodi hiyo. Kuna rekodi nyingine nyingi za timu na za mchezaji mmoja mmoja zinazodhihirisha kuwa performance ya timu ilikuwa juu sana pamoja na kuzidiwa pointi na Yanga.
Leo nakumbushia tu kuwa hadi msimu unapoisha siku ya leo, Simba wanamaliza msimu wakiwa na unbeaten record ya mechi 21, yaani hawajafungwa kwa mechi 21 mfululizo. Hii siyo rekodi ya kubeza hata kidogo. Simba wataiendeleza hii rekodi hadi wapi msimu ujao?
Namalizia tu kwa kusema TFF wafanye juhudi za makusudi kuongeza ushindani katika ligi. Kuna gape kubwa sana kati ya timu 3 za juu na karibia nusu zilizoko chini. Ukitaka kujua hilo, wakati ligi ilipokuwa inaelekea ukingoni, karibia nusu ya timu zilikuwa ziko kwenye hatari ya kushuka daraja wakati Simba na Yanga wanajivunia hizi rekodi za unbeaten. Hili haliko sawa.
Ningependa kuona tunafika wakati ligi ikiwa inapata Bingwa, awe amefungwa mechi hata 4.