Simba hatujapoteza mechi ila performance yetu ilikuwa yakusuasua sana hilo lazima tuliweke wazi.
Hata hizo mechi za unbeaten kuna sare nyingi ambazo hazikuwa za lazima.
Mechi na Singida tukiwa away unaweza ukaona tulivyonusurika kipigo, ule ndio msimu ambao Kibu alikuwa ametepeta to the fullest. Critics walikuwa wanakesha kutu mention kwenye kile kiuzi chao.
Angalia ile mechi na Mbeya City ambayo mchezaji mmoja alipigwa kadi nyekundu, walikuwa pengufu lakini sisi ndio tuliokuwa tunaomba mpira uishe.
Aishi Manula naye kuna sehemu anastahili kuambiwa ukweli aweze kubadilika, kuna magoli ya kizembe alifungwa ambayo yalisababisha kupunguza morale ya timu na kusababisha mechi iishe kwa matokeo tusio yahitaji
Mengineyo
Azam ajiweke fiti asiwe ni mtu wa kugombania nafasi ya pili kila msimu.
Ndio maana mimi huwa natofautiana na baadhi ya mashabiki wanaoosema Simba haisajili kwasababu ya ubahili.
Yusuphu Bakhressa msimu huu ulioisha alisema "sasa nimeamua" alitoa pesa nyingi lakini ndio hivyo msimu umeisha akiwa anagombaniana nafasi ya tatu na Singida.
Natamani Azam waoneshe utofauti kwa kujilipua waje na nguvu kubwa ya kiushindani wakuweza kuonesha kuwa wanahitaji kuwa mabingwa na sio nafasi ya pili.