Simba yamtangaza Hemed 'Morocco' kuwa kocha wa muda (caretaker)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Klabu ya Simba imemtangaza rasmi Hemed Suleiman, anayejulikana zaidi kama Morocco, kuwa Kocha wa muda (Caretaker) kwa mechi za Kimataifa. Uamuzi huu umefikiwa baada ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids, kusitisha mkataba wake, huku Kocha Selemani Matola akikosa nafasi kutokana na kadi nyekundu aliyopewa.

IMG_6283.jpeg

Kupitia taarifa yao, Simba imetoa shukrani kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kumruhusu Kocha Morocco, ambaye pia ni Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), kujiunga na klabu katika kipindi hiki cha mpito. Uongozi wa Simba umeeleza kuwa bado unakamilisha taratibu za kumpata Kocha wa kudumu.
IMG_6284.jpeg

Kocha Morocco ataiongoza Simba katika benchi la ufundi kuelekea mchezo muhimu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United FC, utakaochezwa Septemba 28, 2025.

IMG_6282.jpeg
 
Klabu ya Simba imemtangaza rasmi Hemed Suleiman, anayejulikana zaidi kama Morocco, kuwa Kocha wa muda (Caretaker) kwa mechi za Kimataifa. Uamuzi huu umefikiwa baada ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids, kusitisha mkataba wake, huku Kocha Selemani Matola akikosa nafasi kutokana na kadi nyekundu aliyopewa.

View attachment 3477546
Kupitia taarifa yao, Simba imetoa shukrani kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kumruhusu Kocha Morocco, ambaye pia ni Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), kujiunga na klabu katika kipindi hiki cha mpito. Uongozi wa Simba umeeleza kuwa bado unakamilisha taratibu za kumpata Kocha wa kudumu.
View attachment 3477548
Kocha Morocco ataiongoza Simba katika benchi la ufundi kuelekea mchezo muhimu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United FC, utakaochezwa Septemba 28, 2025.

View attachment 3477542
.......Mtapigwa tena vibaya sana.
 
Morocco tena? Fadlu kaenda Morocco, halafu Simba wanamleta Morocco pia, what a coincidence. Kocha anayeiiweza Simba wakati wa mpito ni Juma Mgunda ila sijui kama Simba wanaweza kuwa na guts za kumrudia tena baada ya kumdhalilisha siku za nyuma.
 
Nitaipenda Simba mpaka kufa.

1. Siwezi kubadili kabila Mimi ni mpare.
2.Siwezi kubadili jinsia Mimi ni mwanaume.
3. Siwezi kubadili rangi Mimi ni black.
4. Siwezi kubadili kimo Mimi ni mfupi.
5. Siwezi kuacha kande Nile wali Mimi ni mpare. (Mwaathu).
 
Dabi ya kariakoo ni lini? Tunataka tumkande simba mara ya saba na ikiwa chini ya Gadiola Mnene part two (Morocco)
 
Back
Top Bottom