Klabu ya Simba imemtangaza rasmi Hemed Suleiman, anayejulikana zaidi kama Morocco, kuwa Kocha wa muda (Caretaker) kwa mechi za Kimataifa. Uamuzi huu umefikiwa baada ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids, kusitisha mkataba wake, huku Kocha Selemani Matola akikosa nafasi kutokana na kadi nyekundu aliyopewa.
View attachment 3477546
Kupitia taarifa yao, Simba imetoa shukrani kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kumruhusu Kocha Morocco, ambaye pia ni Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), kujiunga na klabu katika kipindi hiki cha mpito. Uongozi wa Simba umeeleza kuwa bado unakamilisha taratibu za kumpata Kocha wa kudumu.
View attachment 3477548
Kocha Morocco ataiongoza Simba katika benchi la ufundi kuelekea mchezo muhimu wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United FC, utakaochezwa Septemba 28, 2025.
View attachment 3477542