Simba yamtupia virago KOPUNOVIC,yamleta mbelgiji PIET DE MOL!!!

Soka letu la kuigana sana.
Walianza AZAM kwa kumrudisha mwingereza wao Stewatt.
Sasa ni Simba yangu.
Hans nae ajiandae!!!
 
Soka la Tanzania kuendelea ngumu sana yaani wanatumia hela nyingi kila msimu
 
Soka letu ni la ajabu sana,tunapiga hatua moja mbele kisha tunarudi hatua 9 nyuma then tunakaa na kujipongeza.

Soka letu halijawahi kupiga hatua hata moja kwenda Mbele,

zote zinarudi nyuma.

Cape Verde wametupita,hadi somalia pia watasonga Mbele
 
kila siku huwa nasema bongo hakuna soccer kuna kabumbu
mashabiki na wachezaji wanataka kuiona pepo bila kufa
 
Watakuwa wamemaliza kujenga timu sasa wanataka kupiga bati...
 
Watakuwa wamemaliza kujenga timu sasa wanataka kupiga bati...
Sasa si wangeendelea na fundi aliyekua akijenga?
yani huyu anakuja kuibomoa na kuanza kuijenga upya.
nawashauri yanga wasimuache Hans katu.
siye tushaizoea nafasi ya tatu!!!
 
Sasa si wangeendelea na fundi aliyekua akijenga?
yani huyu anakuja kuibomoa na kuanza kuijenga upya.
nawashauri yanga wasimuache Hans katu.
siye tushaizoea nafasi ya tatu!!!

Hahaha!!!

Fundi mpanga matofali sio sawa na fundi muweka bati...

Ila soka letu bongo dah!!!
 
walichofanya simba ni sawa,kocha alikuwa anataka mkataba wa miezi tisa na kama uongozi ulikataa hilo kwa sababu kama kocha wangempa mkataba wa miez tisa,angeweza fanya usajili wa wachezaji anaotaka yeye na kuwatimua ambao hawataki katika club ya simba,na mara baada ya mkataba wake kuisha angeiacha timu na simba wangetakiwa watafute kocha mwingne.hasara ambayo wangeweza pata ni kocha mpya ambae wangemuajiri angekuta wachezaji waliosajiliwa na kocha mwingne na yeye kama mfumo wake ungekuja kuwa tofauti angeweza watema wachezaji wengne na hivyo kuingizia hasara club.bora walivyomuacha na inaonekana kuna timu inamuhitaji baada ya miezi tisa ijayo
 

Nakuunga mkono mkuu.. Haiwezekani ndani ya miezi 9 kocha apewe 💲 100,000/= mshahara wa zaidi ya 💲 5,000/= kwa mwezi.. Asepe zake.
 
Nakuunga mkono mkuu.. Haiwezekani ndani ya miezi 9 kocha apewe 💲 100,000/= mshahara wa zaidi ya 💲 5,000/= kwa mwezi.. Asepe zake.

yah ni kwel gharama na hasara ambayo wangeweza kuipata club ni kubwa na kuachana nae ndio njia sahihi kwao.nashangaa kuna watu wanawaponda simba kwa kufukuzafukuza makocha bila kujua chanzo nini
 
Timu za wajinga zinaendeshwa kijinga na zinacheza kijinga ndiyo maana zinashindwa kijinga kwa hali hii ligi itaendelea kuwa ya kijinga.
 
Nakuunga mkono mkuu.. Haiwezekani ndani ya miezi 9 kocha apewe  100,000/= mshahara wa zaidi ya  5,000/= kwa mwezi.. Asepe zake.
duh hiyo ni gross au net?
 
mimi kwa hili utani naacha pembeni, mko sahihi kumuacha ...huyu kocha angepimwa akili mngemgundua mapemaaaa, uchizi sio lazima uokote makopo, vile vituko vyake tu vilitosha kumtambua.........eti timu kaifikisha nafasi ya 3 halafu anataka mil.28. kwa mwezi, je angeipa ubingwa??.
angalieni watani msilete chizi mwingine.
 
huwa sikubaliani na maamuzi mengi yanayofanywa na simba lakini kwa hili walikuwa sahihi yule kocha alitaka kuwapanda kichwani kwanza mshahara aliodai ni mkubwa halafu anajifanya ana ofa kibao wakati kuna makocha wengi wazuri wako vijiweni
 
Kaburi kinaletwa na kuchombezwa na Azam. Anadhani Azam atapata pesa nyingi sana. Anaweza kukosa vyote.
Angechukua ubingwa angedai mshahara wa Mourihno kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…