Kama
muanzisha thread hii angekuwa anafuatilia matukio ya kandanda nchini hususan sakata la kocha Goran, asingeianzisha kwa mtindo huu. Kutumia maneno kwamba 'wamemtupia virago' kunaonyesha mwandishi hakutaka kujiuliza hata sababu.
Huyu kocha alikuwa amemaliza mkataba wake kuifundisha Simba. Alipopewa mkataba mpya akakataa kusaini na akaweka masharti ya kiwango kikubwa cha fedha za kusaini cha sh. milioni 100 na mshahara wa sh. milioni 16 kila mwezi. Simba wakamwambia kuwa hela hizo ni nyingi, na wakampa ofa yao ambayo ameikataa. Sasa hapo utasema Simba wamemtupia virago Goran? Basi ni sawa na kusema Yanga wamemtupia virago Mrisho Ngassa kwani sakata lake ni kama hili la kocha Goran!