Best Daddy
JF-Expert Member
- Apr 2, 2019
- 950
- 1,672
Jambo jipya kutokea haimaanishi lile la kale lazima liwe limepotea au limekufa, hivyo naamini nitaeleweka kuwa huu uzi haujamaanisha kuwa Simbana Yanga zimekuwa mbadala(replacement) wa dini na imani za watu. Ila nimekuja kueleza kuwa hizi team zimekua na nguvu ya dini kwa sasa.
Soka ndio mchezo pendwa duniani. Hakuna wa kupinga hilo. Ni kitu pekee ambacho kina watoa machozi wanaume(publicly) kuliko jambo linguine lolote sababu ya passion timu zao.
Vijana wa mjini wanasema mapenzi ya kweli yamebaki kwenye Soka tu. Kwa kuwa ni sehemu ya burudani, mpira ulianza kama passion tu ya watu, baaade tukaanza kusikia watu Wamekuwa machizi wa soka, hasa South America.
Kwa Tanzania kwa kipindi kadhaa kimepita hizi timu zikawa ni obsession wa watu, nimeona baadhi ya malalamiko ya watu hata hapa Jamiiforums kuwa hii jamii inaelekea wapi kwani asubuhi wanaamka tu basi ni michezo.
Maswala ya siasa, jamii serikali wapo mbali, ila kila penye mkusanyiko wimbo ni ule Simba & Yanga. Dunia ya vijana wengi inazunguka katika Simba na Yanga.
Kwa wale ambao sio mashabiki wa hizi timu, wanaona kama mashabiki wa hizi timu wamechanganyikiwa hivi. Wanahisi mashabiki wamekuwa brainwashed. Nataja Simba na Yanga sababu Tanzania mashabiki wengi sio mashabiki wa mpira, bali ni mashabiki na wapenzi wa Simba na Yanga. Mechi yeyote kubwa ambayo haitahusisha Simba na Yanga basi Tanzania inakosa mvuto na kukosa mashabiki kabisa, either ni Timu ya Taifa au mechi nyingine.
Commitment katika timu hizi ni ya hali ya juu. Utetezi kuhusu hivi vilabu ni wa wali ya juu. Watu wamezama kwenye vilabu vyao, kama walivyo wamuuni katika dini, mashabiki hawataki timu yao ikosolewe.
Yeyote atakaye kosoa basi ni adui wao. Na yule atakayesifia basi ndio rafiki yao na ndio yupo sahihi.
Kama ilivyokuwa kuwa ngumu kukosoa katika dini, basi mashabiki hawataki uguse kabisa klabu zao kwa kusema madhaifu yao. Ukitoa madhaifu ya Yanga unaonekana wewe ni Simba, vice versa is true. Hapa ndio kazi ya Wachambuzi Tanzania ilipoanza kuwa ngumu. Ila wengi huwa nawa shauri kama wewe sio shabiki wa kweli wa timu hizi mbili, basi chagua kuwa kwenye kivuli cha Yanga. Maana kamwe huwezi shinda vita dhidi ya mashabiki wa Yanga.
Hapa naamini wengi wanaelewa, kuwa ukiwa katika mapenzi upofu, basi kila kitu unakipokea au kupinga bila tafakuri sahihi.
Kama ilivyo kwa dini, tunapokea taarifa au habari na kuziamini bila kutafakari. Wasemaji wa hizi timu wanalitambua hilo, wanasiasa wanalitambua hilo, hata wachambuzi au waandishi wa habari wa kimataifa wamelitambua hilo. Tunalishwa ujinga sana, tunapokea na kuamini moja kwa moja. Wanatu-enjoy sana, sababu akili zetu tayari zimefunikwa na mapenzi upofu katika zetu.
Mimi pia ni Shabiki wa Simba na Yanga. Hivyo sisemi kama hili ni jambo baya moja kwa moja, ila natamani kuona wakati tunaendelea kushabikia hizi timu tubakize uwezo wetu wa kufikiri na kung’amua mambo. Tusikubali kuwa wajinga wajinga. Mapenzi ya hizi timu yasifanye Rage aonekane kuwa ni sahihi kuwa sisi ni ‘Mbumbumbu’ au Haji Manara kusema kuwa katika mshabiki wa Yanga wenye akili ni wawili tu, tuliobaki ni ‘Mbumbumbu- akili zetu hazifanyi kazi’.
Angalia wanasiasa wanavyotumia mapenzi yetu katika hivi vilabu kupenyeza ajenda zao, kututoa katika agenda za msingi au mambo yenye manufaa katika jamii kwa ujumla.
Tusikubali kutenegneza kizazi ambacho dunia yao inazunguka katika Simba na Yanga. Hii kuanzia vijiweni, hata kwenye media kuanzia asubuhi hadi jioni, watu wanazungumza ni Simba na Yanga. Tuwe tunajipa sabato, tunajipa likizo kidogo. Tuzungumze mambo mengine ya kiuchumi, kijamii hata yale yanayoendelea katika siasa hata kwa uchache, tujaribu kubalance mambo na hiyo ndiyo njia pekee tutatengeneza kizazi bora cha sasa na baadae.
Ukitoa dini kwa Tanzania, basi jambo lenye nguvu kwa sasa ni Simba na Yanga.
Nini matazamo wako kuhusu hili? Je ni kweli Simba na Yanga zimekua na nguvu ya dini mashabiki wa hizi timu? Je ina afya kwa taifa endapo akili ya wananchi wengi inazunguka katika Simba na Yanga? Nini kifanyike au kiboresheshwe?