Simba Yanga wanastahili zaidi kwenye mapato.

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Kuna wakati utamsikia Mtu anakwambia Tanzania kuna Washabiki wengi wa mpira wa miguu,hii si kweli hata kidogo bali Tanzania kuna Usimba na Uyanga usiohitaji hata kushabikia mpira wa miguu au soka.Kwa hali hii ningeshauri kufanyike ubunifu zaidi wa mapato kupitia utajiri huu wa wafuasi waliosheheni kila kona ya nchi,kwa mfano kwa nini Azam wasiweke tozo ya ziada kwenye vifurushi vyao kwa mechi zote zinazohusisha Simba au Yanga,kati ya elfu moja na elfu mbili hivi isiyoathiri gharama kwenye Vibanda umiza vyetu mtaani.Na sehemu kubwa ya tozo hii itakwenda kwa timu husika,na hata pale ambapo Mwenyeji ndiye mnufaika wa mapato basi Simba na Yanga wasiumie bali waone kama huo ni wajibu wao na huo ndio ukubwa.Nchi nyingine huzuia hata kuonesha mechi husika kwenye eneo ambapo mechi inafanyika lengo likiwa kuhakikisha vilabu wanaongeza mapato kwa viingilio.Sidhani kama wenye vibanda umiza watakwazika na utaratibu kama huu kwani wao ni Mashahidi kuwa siku ambayo Simba au Yanga hawachezi wala hawahangaiki kufungua mabanda yao,wao wafaidi na timu zifaidi.
 
Naunga mkono hoja,lazima wafaidi wote.
 
Back
Top Bottom