Simba, Yanga zaingiza Milioni 436

Simba, Yanga zaingiza Milioni 436

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Mechi no.117 iliyowakutanisha Simba na Yanga katika uwanja wa Taifa, imeingiza jumla ya sh. milioni 436,756,000 kutokana na idadi ya watazamaji 49,758 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.

Watazamaji 309 walikata tiketi za VIP A, 1,310 VIP B, 1,533 VIP C, Rangi ya Machungwa (Orange) 9,913 huku viti vya rangi ya bluu na kijani wakiingia watazamaji 36,693.

Mgawanyo wa mapato ya mchezo huo ni VAT 18% sh.66,623.796, FDF timu mwenyeji sh. 17,415,300, FDF TFF sh.7,463,700, Gharama za tiketi sh.11,669,600.

Mgao wa Uwanja sh. 50,037,540.51, Gharama za mchezo sh.28,354,606.29, Bodi ya Ligi (TPLB) sh. 26,686,688.27, TFF sh.20,015,016.20, DRFA sh. 11,675,426.12, klabu ya Simba sh. 115,086,343 (34.5%) huku Yanga wakipata sh.81,727.83 (24.5%)


Chanzo: Shirikisho la Mpira wa Miguu
 
Wataacha kupanga matokeo kwa namna hii?
 
Simba na Yanga zinaifaidisha TFF usitegemee hata siku moja hizi timu kushuka daraja hata mara moja hata kama timu iwe mbovu kiasi gani
 
samahani sina takwimu za kutosha,naomba mnijuze mara ya mwisho yanga kushinda dhidi ya simba ni lini
 
Wataacha kupanga matokeo kwa namna hii?
Mkishaliwa ndio mnaanza kutafuta sababu. Yebo yebo ni mateja wa Mnyama siku zote hata kama Mnyama atachezesha wachezaji 5 kwa 11 wa Yebo Yebo.
 
Hapo hawajataja zile zilizooibiwa na kupitishana ni zaidi ya mil 500
 
Hivi ni kwa nini Mnyama amepata mgao zaidi ya Yebo Yebo. Au ni kwa sababu kampiga kitu Yebo Yebo?
 
Hivi ni kwa nini Mnyama amepata mgao zaidi ya Yebo Yebo. Au ni kwa sababu kampiga kitu Yebo Yebo?

Kwa sababu tulikua wenyeji, na Ndala ni wageni wetu.. Tukawapiga kimoja katika gheto letu, wakasepa kurudi kwao jangwani, huku wanachechemea.
 
Taratibu za mgao wa mkwanja kwa Mnyama anaposhinda kwa wachezaji, nusu ya mapato yanayopatikana mlangoni, hupewa benchi la ufundi pamoja na wachezaji wagawane.. Sasa wachezaji wamepewa milioni 57 wagawane..
Alafu eti mi ndala inasema Mnyama analipa posho ndogo?!
Shame On U Kandambili.
 
Back
Top Bottom