Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamaganda Kabudi amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwaandikia barua klabu ya Simba kuhusu ung'olewaji wa viti uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jana.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini wa Wizara hiyo, imesema barua hiyo itakayoelekezwa kwa Simba iwanakiri na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili gharama za uharibifu huo zilipwe.
Pia, Soma: Jeshi la Polisi latoa tamko baada ya mashabiki wa Simba kuvunja viti Uwanja wa Taifa
Vurugu ziliibuka jana Desemba 15, 2024 katika mechi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baina ya Simba dhidi ya CS Sfaxien, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
"Vitendo vilivyofanyika jana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa havikubaliki na sio vya kimichezo, nakuelekeza Katibu Mkuu kuchukua hatua mara moja. Pamoja na kuwaandikia Simba Sports Club na TFF, wapeni ushirikiano Polisi ili watu wote waliokuwa wanang'oa viti na kuvitupa wakamatwe na wachukuliwe hatua za kisheria, lazima tabia hii ikomeshwe," amesema Profesa Kabudi.
Waziri Kabudi amewataka mashabiki wanaoingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuacha vitendo vya uharibifu wa uwanja kwa kuwa wanasababisha hasara kwa Serikali na kuharibu ubora wa uwanja.