Siyo madogo uwanja umekarabatiwa halafu wajinga wachache wanaharibu kwa mambo ya kipuuzi tu.Lazima serikali ionyeshe mfano ili wengine waache ushabiki wa kijinga namna hiyo.Mambo madogo haya mbona profesa wa majalala anayakuza
Haya majambazi hayastaili HATA kuwa timu ni maharamia,MAHUNI,yana wivu,vijicho.Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamaganda Kabudi amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwaandikia barua klabu ya Simba kuhusu ung'olewaji wa viti uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jana.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini wa Wizara hiyo, imesema barua hiyo itakayoelekezwa kwa Simba iwanakiri na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili gharama za uharibifu huo zilipwe.
View attachment 3177856
Pia, Soma: Jeshi la Polisi latoa tamko baada ya mashabiki wa Simba kuvunja viti Uwanja wa Taifa
Vurugu ziliibuka jana Desemba 15, 2024 katika mechi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baina ya Simba dhidi ya CS Sfaxien, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
"Vitendo vilivyofanyika jana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa havikubaliki na sio vya kimichezo, nakuelekeza Katibu Mkuu kuchukua hatua mara moja. Pamoja na kuwaandikia Simba Sports Club na TFF, wapeni ushirikiano Polisi ili watu wote waliokuwa wanang'oa viti na kuvitupa wakamatwe na wachukuliwe hatua za kisheria, lazima tabia hii ikomeshwe," amesema Profesa Kabudi.
Waziri Kabudi amewataka mashabiki wanaoingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuacha vitendo vya uharibifu wa uwanja kwa kuwa wanasababisha hasara kwa Serikali na kuharibu ubora wa uwanja.
View attachment 3177852
Mkuu kesho nitakukuta kwenye nyuzi za siasa unalalamika ccm wanaminya uhuru wa chadema🤣🤣🤣😅Wafungiwe kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa, wachezee Bunju
Ndugu CAF hawatumii ripoti za Serikali yenu kufanya maamuzi.Waziri mshenzi huyo, ripoti ya POLISI ilieleza kuwa waarabu ndiyo walioanzisha kuwapiga mashabiki wa Simba kwa viti, wanasimba nao wakavirusha kujibu mapigo.
Huyo waziri anaifanya habari hii ionekane kuwa Simba ndiyo wakorofi. Simba Haina Sifa yoyote mbaya katika eneo la mashabiki, haijawahi kufungiwa. Anaichafua nchi yake mwenyewe kwa kukosa weledi. Alinde maslahi ya taifa badala ya kutoa matamko yanayoweza kutumiwa kama rejea baadae ya kuiharibu taswira ya mpira wetu.
😀😀😀,Uko shirikisho refa ana hongwa Dola 200 na Carton Moja ya MO energy baada ya mechi tuna Rudi kukarabati uwanja kwa mamilioni ya shilingi.
Kunywa maji mengi na upumzikee, PoleeeeeeeeSimba wamesha lalamikiwa na vilabu vingi vinavyo kuja kucheza Benjamin Mkapa, Uwanja wa Taifa CAF wanauangalia kwa jicho la karibu kutokana na timu Nyingi kulalamika hasa zichezapo na Simba.
Kuanzia Ulozi, Marefa na Sasa vurugu za Mashabiki.
Ili ku uweka Uwanja sehemu salama kabla Rungu halijatufikia kama Taifa, Simba mechi zao zihamishiwe Karume pale Tff.
Mechi za shirikisho hazina Tija yoyote katika mpira wetu Sasa Taifa lisi ingie aibu na kuendelea kupata hasara kwa vitu vya kipuuzi.
Uko shirikisho refa ana hongwa Dola 200 na Carton Moja ya MO energy baada ya mechi tuna Rudi kukarabati uwanja kwa mamilioni ya shilingi.
Punguza hasira mkuu , mbona yanga mtashinda tu.Ikiwezekana walipishwe mara mbìli zaidi
Kuna vituko ila mnaokata mauno ni uto.Yaani shirikisho Kuna vituko, Refa katoka Madagascar kahongwa kolekole mmoja na pakacha la Nazi mdondo, anachezesha mpira mpaka dk ya 100.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamaganda Kabudi amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwaandikia barua klabu ya Simba kuhusu ung'olewaji wa viti uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jana.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini wa Wizara hiyo, imesema barua hiyo itakayoelekezwa kwa Simba iwanakiri na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili gharama za uharibifu huo zilipwe.
View attachment 3177856
Pia, Soma: Jeshi la Polisi latoa tamko baada ya mashabiki wa Simba kuvunja viti Uwanja wa Taifa
Vurugu ziliibuka jana Desemba 15, 2024 katika mechi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baina ya Simba dhidi ya CS Sfaxien, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
"Vitendo vilivyofanyika jana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa havikubaliki na sio vya kimichezo, nakuelekeza Katibu Mkuu kuchukua hatua mara moja. Pamoja na kuwaandikia Simba Sports Club na TFF, wapeni ushirikiano Polisi ili watu wote waliokuwa wanang'oa viti na kuvitupa wakamatwe na wachukuliwe hatua za kisheria, lazima tabia hii ikomeshwe," amesema Profesa Kabudi.
Waziri Kabudi amewataka mashabiki wanaoingia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuacha vitendo vya uharibifu wa uwanja kwa kuwa wanasababisha hasara kwa Serikali na kuharibu ubora wa uwanja.
Tulipe tu labda itawatoa mkiani mwa kundi lao😁Niwaeleze ukweli tuu hakuna fine simba itakayolipa ...
WalipeHawa wahuni mechi ijayo wacheze bila mashabiki.