Simba yavuta mido mnaijeria

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
LICHA ya kutimiza idadi ya wachezaji 12 wa kigeni, Mwanaspoti limebaini Simba inaendelea na mikakati ya chinichini ya kumalizana na mido mpya kutoka Nigeria. Lakini wanafikiria pia kumalizana na Mudathir Yahya.

Awali mabosi wa Simba pamoja na benchi la ufundi walikubaliana kufunga zoezi la usajili baada ya kumpata straika Mserbia, Dejan Georgijevic kama Mwanaspoti lilivyokuwa likikueleza.

Lakini baada ya kufanya tathimini ya pamoja na benchi la ufundi katika mechi mbili za kimashindano na moja ya kirafiki wamebadili maamuzi na sasa kabla ya dirisha la usajili kufungwa Agosti 31 watashusha kitu kwa siri sana.

Mwanaspoti linajua wamekubaliana kusajili kiungo mpya wa mkabaji na mezani wana majina mawili chaguo la kwanza kiungo mkabaji wa Kwara United kutokea Ligi Kuu ya Nigeria, Afeez Nosiru.

Nosiru anapewa nafasi kubwa ya kusajili na anaendelea na mazungumzo na Simba inayofikiria kumtoa kwa mkopo Victor Akpan kumrejesha Coastal Union.

Mbali na Nosiru pia mezani Simba ina chaguo la pili, kiungo wa zamani wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Mkenya Teddy Akumu ambaye kwa sasa ni mchezaji huru. Lakini nafasi yake ni finyu.

Simba kama itashindwa kumalizana na Nosiru itahamia kwa Akumu aliye huru lakini lengo ni kuhakikisha mtu anatua kabla dirisha halijafungwa

Nosiru usajili wake ukikamilika anakuwa mchezaji watano anayecheza eneo la kiungo wa ukabaji kwani atawakuta, Jonas Mkude, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Erasto Nyoni.

Katika soka la ushindani Nosiru kabla ya kujiunga na Kwara United amewahi kupitia Niger Tornad msimu 2020-21, zote kutokea Nigeria.

Inaelezwa kama mambo yatakwenda vizuri kama yalivyo wakati huu muda wowote kuanzia sasa Nosiru anaweza kuwasili nchini akatambulishwa katika kikosi hicho chenye kiu ya kufanya vizuri msimu huu.

Meneja habari wa Simba, Ahmed Ally alisema dirisha la usajili bado lipo wazi na kama kutatokea mapendekezo ambayo kocha, Zoran Maki atakuwa anahitaji hawatashindwa kumtimizia haraka iwezekanavyo.



ISHU YA MUDATHIR

Aidha mabosi wa Simba wamefanya mawasiliano na kiungo wa zamani wa Azam, Mudathir Yahya lakini inaelezwa kwamba ni kama anadengua kwani muitikio wake ni mdogo.

Ingawa Simba wamepanga kiungo huyo aliyewahi kukipiga Singida United awe sehemu ya wachezaji wa ndani ya kikosi hicho kinachoongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa tofauti ya mabao ya kufunga baada ya raundi ya kwanza
 
Mhhhhhh Bado naendelea Julia na kamati ya usajili.

Huyu MZUNGU mshambuliaji anatafuta nini Simba????

Banda nae auzwe tu.

Kumtoa Akpan BONGE la KOSA Akpan ni ni Backup nzuri ya ya kanute.

NAIONA KAMATI IKIENDELEA KUFAVNYA MAKOSA.
SIMBA AJIRINI MKURUGENZI WA UFUNDI ACHENI USHAMBA.

# KUMTOA AKPAN NI MAKOSA MAKUBWA SANA.
 
Sijawahi mkubali mudathir yahaya
Kazi kweli kweli umkatae akpan na mkude pamoja na kapama umuingize mudathiri na dejan ila kocha wa simba kajua kunyoosha watu msimu huu
 
Wakati mnamsajili huyo Victor Akpan, niliwaambia humu ni average player! Ila kwa bahati mbaya mlinipuuza. Hata pale nilipohoji kama ana baraka za kocha mpya, majibu yalikuwa ni ya kidwanzi tu.

Wiki chache baadaye, ukweli unaonekana.
 
Poor scouting, poor performance.
Yajayo yanasononesha.
 
Mudathir ni wa nini...mbona kama Simba sasa hivi kuna Mtu anatia shinikizo la kusajili Watu anaowataka yeye?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…