Carlos The Jackal
JF-Expert Member
- Feb 6, 2017
- 25,725
- 78,589
Huku mtaani kuna kundi la watu wengi hawana ajira na wamekuwa wakipambana juu chini kutafuta ajira wakiwemo Vijana.
Wakati huohuo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene hivi karibuni alinukuliwa akisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na Tume ya Utumishi wa Umma nchini ni kuwa zaidi ya Asilimia 40 ya Watumishi wa Umma hawafanyi kazi licha ya kulipwa mshahara kila mwezi.
Ukiangalia anchokisema Waziri, inamaanisha hii asilimia 40, maana yake wahusika wataenda hivyohivyo hadi kustaafu kwao na hivyo watakuwa wamelisababishia hasara Taifa.
Kuendelea kuwabeba watu hao huku Watanzania kila siku wakilalamikia taasisi za Umma kutokuwa na Uwajibikaji, Je, Serikali inamkakati wa kuwafanya hao 40% wawe wachapakazi, wenye uwezo wa kazi na waache uvivu?
Kwanini hiyo 40% wasiwekwe pembeni? Wakaajiriwa wengine? Kwanini ajira zisiwe za Mikataba ya miaka Kadhaa?
Hivi hata kama hauna akili na hujasoma, kwamba wee una Kampuni yako, umeajiri watu , ukagandua kwa utafiti kabida kuwa baadhi yao ni wazembe, Wavivu, wasiokuwa na ujuzi wa kazi zao, bado utaendelea nao tu? Wakati huko nje kuna watu wanatafuta Ajira na wana uwezo wa juu?
Pia soma ~ Simbachawene: Ripoti zinaonesha zaidi ya 40% ya Watumishi wa Umma Tanzania hawafanyi kazi