Simbachawene: Kama zile 5-1 zimetokana na Rushwa, Simba mkaripoti TAKUKURU Temeke

Simbachawene: Kama zile 5-1 zimetokana na Rushwa, Simba mkaripoti TAKUKURU Temeke

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema kama Klabu ya Simba inaamini kupoteza kwa magoli 5-1 dhidi ya Yanga kumechangiwa na mazingira ya rushwa basi taarifa hiyo ikaripotiwe Ofisi ya TAKUKURU Temeke, Dar es Salaam.

Awali, Mbunge Festo Sanga alihoji mpango wa Serikali kukabiliana na rushwa baada ya kuwa na tetesi za madai ya rushwa katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa.
 
Bongo kila kitu hovyo, soka hovyo, viongozi hovyo wanataka kujadili vitu vya hovyo na kuacha vya maana.

Timu yetu ni mbovu na tumefungwa na waliokuwa bora sasa shida iko wapi, tukubali, tutengeneze timu. Mbona toka msimu uliopita tulikuwa tunalalama timu mbovu, ukaja usajili tukalalama usajili ni mbovu, sasa walitegemea maajabu gani, kama mpaka sisi tu tumeona timu mbovu unategemea nini kukutana na yanga wazima.

Tena hii fedheha ilikiwa itukute mwa al ahly ni vile tu wale mambwiga kosa kosa zilikuwa nyingi.
 
Msimu wa 2020/21 walifungwa na Prison na baadae Mtibwa viongozi wa simba wakaenda kuwafukuza wapishi wawili eti kwenye simu zao walikua na namba ya Senzo. Leo simba wana wa simamisha wachezaji kisa kufungwa goli 1-5 na YANGA. Kutaka kuaminisha washabiki wao kuna hujuma hii ni mbinu yao siku zote kutaka kupunguza kelele za washabiki.
 
Ameweka msisitizo kabisa “Kama zile tano zimetokana na rushwa !” 😁😁😁😁
 
Simba kawa nyau kilichobaki ni kulialia tu
 
Wanaharibu michezo hawa, na kuzalilisha watu na kuvunja moyo wachezaji wa simba.
Hawa Watu Wa Serikali Ni Wapuuzi Sana, Michezo Ni Burudani, Afya, Ajira
Vinafungwa Vilabu Vikubwa Ulaya Na Idadi Kubwa Kuliko Ya Simba
Huwezi Sikia Ujinga Huu Wa Tanzania Ukizungumzwa


Wanasiasa Waache Michezo Ijiendeshe
 
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora ameishauri klabu ya Simba kwenda TAKUKURU kama wanahisi Goli 5-1 ni matunda ya Rushwa.

Mh George Simbachawene amelieleza Bunge leo.

Source: TBC
 
Huyu Simbachawene kama angekuwa anajua PCCB ipo na inafanya kazi angewaambia kwanza waanze kumchunguza Mwigulu.

Hakuna mchezaji wa Simba aliyepewa rushwa, ni watu wenye ufinyu wa akili wanaoamini hivyo.
 
Hizi shutuma zinahitaji uthibitisho kwani zinagusa HISIA za makundi mengi ndani ya Jamii, wanaume, wanawake, wasomi, viongozi, watoto, sponsors, media, authorities, international, wachezaji wadogo wanaokuwa ktk football industries.

Si jambo dogo dogo hata kidogo, kama kuna any primary evidence hata kama ni ndogo kiasi DOLA I- take very serious measures, very serious..
For soccer health.

Kama kuna any Attempt by YANGA, this to be taken as an example, but if there is any mazingira. Even Any mazingira. Narudia.

NBC LEAGUE ilishaanza kupata HESHIMA, lakini kwa haya MADOA.
 
Back
Top Bottom