Kwa uzoefu wangu kwa serikalini lazima kuwe na mzigo tena asilimia ni zaidi ya hiyo .Sababu ni ndogo ndogo tu wala sio kubwa sana.
Wafanyakazi wengi wa serikali ni watu waliojihakikishia mshahara then wanatafuta njia ya kwenda mbele zaidi ,ishu kama kwenda kusoma ni bora wafute ; kazini kwetu napiga vitengo vitatu kwa pamoja ,hao wawili wameenda kusoma tena mwaka huu na wengine wanaenda .Kiufupi ufikishaji wa huduma kama ilivyokusudiwa ni zero kila mtu anatafuta vyeo.
Mlundikano wa wafanyakazi sehemu moja kutokana na sababu za kimazingira ,watu hupenda kujilundika mkoa fulani kuliko mwingine .Matokeo yake sehemu za mijini watu ni wengi mpaka hawafanya kazi wengine meanwhile huko kijijini hakuna watu .
Ruhusa za hovyo hususani hizi za kuumwa ,kuuguza mzazi ,mke au mtoto ni hatari sana mbaya zaidi kama mzazi itabidi mtu aende mkoani huko maana hafanyi kazi mkoa waliopo wazazi wake. Haya mambo ni kawaida sana waliokuwa na familia ni changamoto ,mtu miezi yuko Muhimbili kuuguza mtoto wake sio rahisi kuepuka mambo hayo.