Simbachawene: Serikali kuangalia upya utaratibu wa kuanzisha Makanisa, Wachungaji watapaswa kuwa na Shahada ili kupunguza "Vibanda Imani"

Simbachawene: Serikali kuangalia upya utaratibu wa kuanzisha Makanisa, Wachungaji watapaswa kuwa na Shahada ili kupunguza "Vibanda Imani"

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa mambo ya ndani Mh Simbachawene amesema kufuatia vifo vya watu 20 kwenye Huduma ya Mwamposya huko Moshi, serikali itaangalia upya utaratibu wa kusajili hizi Huduma.

Simbachawene amesema Wachungaji wanaoanzisha Huduma za kiimani watapaswa kuwa na shahada ili kupunguza " Vibanda Imani" vilivyozagaa kila kona.

Rwanda wamefanikiwa kudhibiti Vibanda Imani kwa kutumia utaratibu huu, amesisitiza Simbachawene.

Source Clouds tv!
 
Dini ni biashara inayolipa sana!

Ukitaka kumchota akili mnyama,mpe chakula;ukitaka kumchota akili binadamu,mpe imani.

Imani sometimes huzaa ujinga, na ujinga kwenye imani huzaa upofu!

Hiyo habari ya kuwa na shahada wala haitasaidia.
 
Shida sio Elimu, wote wanaweza Kuwa na Elimu na wakaharibu, Mwamposa hana Elimu?
UKO SAHIHI

Waziri haelewi anachoongea nafikiri alikuwa aongee opposite kuwa waumini wa dini ndio wawe na digrii za dini sio viongozi wa dini.Kwa sababu kama ni uelewa labda waumini ndio hawana

Sababu mtu kama mfano TB JOSHUA au Mzee mwasapile wa kikombe cha babu elimu hawana lakini maprofesa na ma doctor walienda kukinywa NA kWA TB JOSHUA NIGERIA HUFURIKA KIBAO.Imani ni kitu complicated

Yeye asisitize tu usalama maeneo ya ibada kuwa viongozi wa dini wahahakikishe kuna usalama kwenye maeneo yao ya ibada.Hayo mengine ya wanaabudu nini awaachie wenyewe kama watakanyaga mafuta au mavi ya kiongozi wa dini shauri yao
 
Waziri wa mambo ya ndani mh Simbachawene amesema kufuatia vifo vya watu 20 kwenye Huduma ya Mwamposya huko Moshi, serikali itaangalia upya utaratibu wa kusajili hizi Huduma.

Simbachawene amesema Wachungaji wanaoanzisha Huduma za kiimani watapaswa kuwa na shahada ili kupunguza " Vibanda Imani" vilivyozagaa kila kona.
Rwanda wamefanikiwa kudhibiti Vibanda Imani kwa kutumia utaratibu huu, amesisitiza Simbachawene.

Source Clouds tv!
Walikuwa wapi siku zote eti Masanja nae Pastor[emoji134][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom