Simbachawene VS Bashungwa: Vijana tumejifunza nini?

Hii ni mitihani ya level tofauti kwa nyakati tofauti kabisa.

Huwezi kumpima Bashungwa kwa tukio la Oktoba 29 kipindi ambacho mamlaka za juu yake zilikuwa zimejiandaa kwa lolote na zimejawa na jazba, hasira na kila aina ya hofu kwa kulinganisha na D9 ambapo mamlaka za juu ya Simbachawene zilikuwa kwenye harakati ya kusaka huruma ya nje na ndani, hofu ya kuendelea kutoaminika, na kupoteza madaraka yao.

D9 ilikuwa lazima yafanyike yaliyofanyika kwasababu kilichofanyika ndicho ambacho mamlaka zilikitaka na Mo29 kilifanyika kilichofanyika kwasababu mamlaka zilitaka kifanyike hivyo hivyo
 
Mbona tuna wazee wa ovyo.
Muriro.
Charamira.
Babu wa tiktok.
Samuya.
Jaji wa tume ya uchaguzi.
 
Bashungwa bado anapumua???
 
Hao wako hapo kwenye nafasi zao kama maboya tu, maagizo yanatoka kwa rais na genge lake. Mfano halisi wa kuwa hao mawaziri ni maboya tu, juzi Simbachawene kasema watu wakamatwe kwa kufuata taratibu za nchi, mbona bado wanakamatwa kwa mtindo huo huo na hajachukua hatua yoyote? Ukiwa chawa lazima utumie akili yako pia kusema uhalisia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…