Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbuge wa Jimbo la Kibakwe George Boniface Simbachawene amesema kuwa amepokea kwa mikono Miwili na kwa Moyo wa Shukrani Uwamuzi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya Kutengua Uteuzi wake katika nafasi hiyo.
Aidha Simbachawene amesema kuwa, Rais anayo Mamlaka ya kumteua mtu yeyote katika nafasi yoyote au kumtengua mtu yeyote katika nafasi yoyote nia ikiwa ni kufanikisha dhima yake katika kuwaletea Maendeleo Watanzania.
Simbachawene ameyasema hayo jana januari 24, 2026 alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Pwaga katika jimbo la Kibakwe mara baada ya kuwasili Jimboni hapo lengo ikiwa ni kutembelea na kukagua Miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ndini ya jimbo hilo.
Aidha Simbachawene ameahidi kuendelea kuwa mtiifu na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT. Samia Suluhu Hassan atika nyanja zote ili kuwaletea maendeleo Watanzania hususani wananchi wa Jimbo la Kibakwe.
Soma pia

- Makonda ateuliwa kuwa Waziri wa Habari, Simbachawe atenguliwa Uwaziri wa Mambo ya ndani ya Nchi
- Simbachawene: Rais Samia ameagiza mabadiliko Polisi ili kurejesha mahusiano mazuri na wananchi