Nani amemuelewa huyu kaka blaza?Inasikitisha kuona jinsi baadhi yetu tunavyoendelea kulalamika wakati tumepewa fursa nzuri ya kufurahi na kupongezana kwa haya maendeleo ya msingi.
Tunapaswa kuwa tunafurahi pamoja na ndugu zetu walio wateja wa SimbaNET bila kuwa na wivu wala usongo, kwani katika siku za usoni wenzao wengine tutawafuata pia katika huduma hii ya Internet kupitia marine cable. Na bei zitashuka tu, lakini lazima tuanze hapa kwa kuunganishwa kwenye mtandao, ndipo tupate kuliangalia suala la bei.
Hongereni sana wanaSimbaNET kwa kufanikiwa kutufungulia sote kiingilio cha SEACOM!
Utaweza kuona ila nilazima uisubirie kwa mda kidogo.Yo Yo Vp hapo r u in? Make we na Melo ndo wataaluma wetu hapa tunategemea ushauri mkubwa kutoka kwenu. Hiyo sijui 80/80 itaniwezesha kuona clips za Youtube kweli?
Mkuu Yo Yo, Wewe Wasema.
karibu sana.
Nani amemuelewa huyu kaka blaza?
Duh,
Basi tena!
Mtsimbe, kwanza samahani kuwa kwenye picha nilizoweka zote nilisahau kuweka ambayo unaonekana, kumradhi kwa hili na nimeambatanisha picha yako chini. Mtsimbe ni wa kwanza kushoto (nadhifu 🙂 )
Pili, vipi mimi nahitaji atleast 512kbps, naweza kupata kwa bei gani? Naweza kupata wapi maelekezo au price list kwa lugha ya kigeni?
Ahsante
Kumbe huu mkonga haujapunguza kitu wabongo bana kwa kupenda super profit dah.
Sasa sijui hawa walioleta mkonga ndo wanawakamua au hawa maagent ndo mnatukamua maana bongo bana.
d=Maxence. nitumie kweny barua pepe nitakupatia. Kwa sasa si rahisi kwangu kuanika Price List yote hapa kwa sababu za kibiashara na kiushindani. lakini tumepunguza bei zetu kwa zaidi ya asilimia 50%.
wee acha tu maana raisi alituambia ati gharama zitapungua saaaana more than 70% lakini naona kama ndio zimeongezeke..au Sactus anakula cha juu?joking
lol umemtafutia balaa.....PM yake imeshajaa shoriiiizi
Naam, hakuna anayefanya biashara ili apate hasara!
Naamini kabisa kwamba mkiweka mkakati wa nguvu kuwafikia wateja wengi mapema, bei yenu ya kuuzia ingekuwa ndogo hata kuipiku hiyo rate huko Kenya na bado mkapata faida. Badala yake mmeamua kwenda na strategy tofauti. Of course mna hiyari ya kufanya mtakavyo.
Kwa bei hii unayotueleza, I cannot see you buying another fiber pair, kwani hiyo 155 Mbps itawachukua muda mrefu sana kuigawa. Usisahau, kuna kundi kubwa la wanafunzi ambao watakuwa wanapata fast & free Internet vyuoni.
Ndugu,speed bado ni ile ile ambayo nilikuwa naipata siku zote,sijaona mabadiliko yoyote kwenye speed.Labda tu subirie tuone kama watatuongezea bandwidth...mimi nilichukua speed ya 128 kbps sijui wataniongezea au la.
mkuu kwenye marketing kuna strategies ambazo lazima uwe mjanja ku hit consumer wako....kuna kitu wanaita skmiming hii ni pale unapoingia kwenye soko kama producer au seller unaanza na bei kubwa ambapo bidhaa yako utakapo i launch onto a market.....marketer wanafanya hivi baada ya kuona demand ya product yao is very high mind you skimming haidumu kwa mrefu pale demand inapoanza kupungua basi lazima washushe bei....
hii ina apply sana sana kwenye bidhaa zile ambazp haiathiriki na mabadiliko ya bei wenyewe wanaita inelasticity of demand...mfano hai ni designer-label clothing.....
nafikiri hawa ISP wamejisahau ku deal na pricing penetration.....mtu wa kawaida kama mie nianaetaka 2Mbps siwezi ku afford kulipa milioni 4 kwa mwezi.....otherwise tanzania tutabaki vile vile as zamani hatutaona faida ya fiber optic wires.....
Ahsante kwa ufafanuzi wako.JOSM;
Kama wewe ni mteja wetu:
VSAT Latency kwenda UK ilikuwa zaidi ya 600 Milliseconds
Sasa hivi latency kupitia Mkongo wa bahari ni kati ya 250-300 Milliseconds
Kwa hiyo speed imeongezeka zaidi ya mara mbili.
Kuhusu kuongezewa capacity: Kama uko DSM nilitegemee hilo, bila ya shaka utaongezewa. Sasa hivi Ma-Engineers wetu wanalishughulikia hilo na in a short time you should be Ok.
Jamani hawa ni SimbaNet kuna kampuni zingine zaidi ya sita ambazo nazo itaungwa kwenye SEACOM..Tusubiri hao na tuone ushindani wa kweli...as consumers we will always go for the cheapest and fastest provider!!
I hope TCRA wako upande wa consumers on this one lasi ivyo tutaliwa kama tunavyoliwa kwenye GSM networks!!
Inasikitisha kuona jinsi baadhi yetu tunavyoendelea kulalamika wakati tumepewa fursa nzuri ya kufurahi na kupongezana kwa haya maendeleo ya msingi.
Tunapaswa kuwa tunafurahi pamoja na ndugu zetu walio wateja wa SimbaNET bila kuwa na wivu wala usongo, kwani katika siku za usoni wenzao wengine tutawafuata pia katika huduma hii ya Internet kupitia marine cable. Na bei zitashuka tu, lakini lazima tuanze hapa kwa kuunganishwa kwenye mtandao, ndipo tupate kuliangalia suala la bei.
Hongereni sana wanaSimbaNET kwa kufanikiwa kutufungulia sote kiingilio cha SEACOM!
Utaweza kuona ila nilazima uisubirie kwa mda kidogo.
Mkuu tuporomoshee bei zenu basi tuzijue ambao tulikuwa hatuzijui ili tusinunue mbuzi kwenye gunia.