Simiyu: David Kafulila apiga marufuku usafirishaji abiria kwa magari madogo yanayotambulika kama "Mchomoko"

Simiyu: David Kafulila apiga marufuku usafirishaji abiria kwa magari madogo yanayotambulika kama "Mchomoko"

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869

13 July 2022​

Simiyu, Tanzania,

MCHOMOKO"​

thumb_1406_800x420_0_0_auto.png


Posted On: July 13th, 2022


RC SIMIYU APIGA MARUFUKU MICHOMOKO KUBEBA ABIRIA.

MKUU wa mkoa wa Simiyu,David Kafulila amepiga marufuku kwa magari madogo ya abiria yanafanya biashara ya kusafirisha watu maarufu kwa jina la Michomoko katika mkoa huo kuacha mara moja kwani wanakiuka masharti ya leseni zao.

Pia magari hayo yamekuwa ndiyo chanzo cha ajali katika mkoa huo na kusababisha kupoteza maisha ya watu na kuwapatia vilema vya maisha.

Rc Kafulila amefikia Uamuzi huo kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo ya Magereza nje kidogo ya mji wa Bariadi ambapo watu watano waliopoteza maisha na wengine kumi na moja kujeruhiwa.

Kafulila ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo ambapo alisema vyombo hivyo vya usafiri pamoja na wamiliki wake wamekuwa hawafuati maelekezo ya serikali ikiwemo mamlaka ya udhibiti usafirishaji wa ardini (LATRA).

Amesema pamoja na hatua zingine za kiutawala zinazoendelea kutokana na ajali hizo yeye kama mkuu wa Mkoa aamua kufanya maamuzi ya kimfumo kwa maana ya kwamba hizo gari zinasajiliwa kwa ajili ya kufanya kazi na zinafanya kama daladala (tax).

Amesema inafahamika kwamba Ili gari zifanye kazi kama daladala, kuna utaratibu wake ikiwemo rangi na alama pamoja na namba ili kusudi likitokea tatizo lolote lile iwe rahisi kufahamika na kuziratibu.

"Wamiliki na waendeshaji wa michomoko kwa zaidi ya nusu mwaka wameshapewa maelekezo ya taratibu za kufuatia Ili kusudi waendelee na kazi hizo za usafirishaji lakini mpaka Sasa hakuna gari iliyotekele hayo maelekezo Ili isajiliwe" amesema Kafulila.

Amesema kuwa kutokana na ajali hizo zimekuwa zikighalimu maisha ya watu, kusababisha ulemavu na kutokana na ukubwa wa jambo lenyewe nimeelekeza kuanzia leo gari zote aina ya michomoko hazipaswi kuonekana barabarani zikifanya biashara ya usafirishaji wa abiria mpaka itapo amliwa vinginevyo.

Aidha ametoa wito kwa wamiliki wa magari ya abiria na wawekezaji katika sekta ya usafirishaji wake katika soko la Simiyu kwa huo ni usafiri salama zaidi na kunauhitaji mkubwa wa magari ya abria Ili kuziba ukosefu wa usafiri.

Source : RC. KAFULILA APIGA MARUFUKU USAFIRISHAJI ABIRIA KWA MAGARI MADOGO YANAYO TAMBULIKA KAMA
 
Hatua nzuri kudhibiti ajali, soko la usafirishaji abiria limevamia na kuwa vurugu tupu.

Kuanzia hawa usafiri wa mchomoko, bodaboda, bajaj idadi ya vyombo hivi imekuwa kubwa kupita mahitaji kwa kuwa mamlaka za eneo husika na pia LATRA kutoa leseni za usafirishaji bila kuwa na ukomo wa idadi hivyo kuwepo ushindani baina ya waendeshaji na pia wamiliki wa vyombo kuwawekea lengo madereva ambayo kiuhalisia kwa kufuata soko lililopo la abiria inapelekea waendeshaji kuvunja sheria za usalama za barabarani na sheria za usalama za abiria.

Mikoa yote Tanzania ifuate uamuzi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu ili waweze kwa pamoja na jeshi la Polisi na mamlaka kama za LATRA na halmashauri za wilaya waweze kudhibiti uholela wa uendeshaji wa biashara hii ya usafirishaji abiria ambao unasababisha ajali kutokana na ushindani usio na uhalisia wa mahitaji ya usafiri salama wa abiria.


Video : Mfano wa barabara kuu Tanzania Kahama Geita na Nzega.

 
Sasa siku zote alikuwa wapi! Mpaka ajali itokee ndiyo apige marufuku!
 
Nyingi ni probox, ubeba hadi watu 10
Kule Ngara hiyo Probox inabeba abiria mpaka 20, nimeona kwa macho yangu, sio ya kuambiwa, na pale Mlima Knine wanashuka kama ndegr ya ardhini. Naunga mkono kuzuiliwa kwakweli.
 
Events driven.. usafir gan hauna ajali hapo Musoma Bariad
 
Rc Kafulila amefikia Uamuzi huo kufuatia ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo ya Magereza nje kidogo ya mji wa Bariadi ambapo watu watano waliopoteza maisha na wengine kumi na moja kujeruhiwa.

]

Matamko kazini
 
LATRA nao wamekuwa wasikivu, yatoa tamko.

Maana ilikuwa Ni vurugu usafiri wa umma kutoratibiwa.

Bajaj, bodaboda, noah, pro box, matrekta yalikuwa ndiyo yamesajiliwa kwa uwingi kupita kiasi kuwa usafiri wa umma na kuua usafiri wa mabasi makubwa ktk njia kuu na mijini.

Lazima kila kitu kinachotumiwa na umma kuratibiwa siyo kusajiliwa ki-uholela.
 
15 July 2022
Bariadi, Simiyu
Tanzania

LATRA yatoa tamko mbele ya waandishi habari

 
Back
Top Bottom