PreGE2025 Simiyu: Luhaga Mpina anusa kufanyiwa figisu, ataka kampeni za wazi Kisesa

PreGE2025 Simiyu: Luhaga Mpina anusa kufanyiwa figisu, ataka kampeni za wazi Kisesa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, amesema kuwa licha ya muda wa kampeni za ubunge ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) bado kutokuwa rasmi, watia nia katika jimbo hilo wanapaswa kuruhusiwa kufanya kampeni mchana kweupe badala ya usiku.

Mpina amesema kuwa kampeni zinazofanyika kwa kificho nyakati za usiku haziwezi kuwasaidia wagombea, akisisitiza kuwa ana uzoefu wa miaka 20 katika siasa na anafahamu mbinu zinazoweza kusaidia mgombea kushinda.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Hakuna haja ya kufanya kampeni za mafichoni usiku, waachwe wafanye mchana kweupe ili wapambane kwa uwazi,” alisema Mpina, akiongeza kuwa kampeni za siri zinaweza kuwathiri wagombea katika uchaguzi mkuu ujao.

Kauli ya Mpina inakuja wakati ambapo mbio za kuwania ubunge katika maeneo mbalimbali nchini zinazidi kushika kasi, huku wagombea wa CCM wakijiandaa kwa mchakato wa kura za maoni ndani ya chama hicho.

 
Back
Top Bottom