DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Katika kesi hiyo ya jinai Na. 12270/2025 iliyosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi, Enos Misana, upande wa mashtaka uliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Violent Mushumbusi, pamoja na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Insp. Vedastus Wajanga.
Kwa mujibu wa maelezo ya mashitaka, tukio hilo lilitokea mwezi Oktoba 2023, usiku, katika nyumba ya mtuhumiwa, ambapo alikwenda katika chumba alichokuwa amelala mtoto huyo pamoja na watoto wenzake, kisha kumbaka na baadaye kumpa ujauzito. Mtoto huyo alibainika kuwa ni ndugu wa mke wa mtuhumiwa.
Baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alikamatwa Januari 26, 2025, kwa ushirikiano wa Mtendaji wa Kijiji cha Mwanundi, Mtendaji wa Kata ya Sengwa, Kamanda wa Sungusungu wa Kijiji hicho, pamoja na walimu wa Shule ya Msingi Mwanundi, na kisha kufikishwa katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Maswa.
Mtuhumiwa alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa moja la ubakaji kinyume na Kifungu cha 130(1), 2(e) na 131(1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 (Marejeo ya mwaka 2022).