Pre GE2025 Simiyu: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Simiyu: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

WanaJF,​

Mada hii itakuwa na 'Updates' za Matukio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Simiyu. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.


Simiyu.jpg

Mkoa wa Simiyu ni mojawapo ya mikoa ya Tanzania, ulioko kaskazini-magharibi mwa nchi. Mkoa huu ulianzishwa rasmi mwaka 2012 baada ya kugawanywa kwa Mkoa wa Shinyanga. Simiyu umepewa jina kutokana na mto Simiyu ambao hupita katika maeneo yake. Makao makuu ya mkoa huu yapo mjini Bariadi.

MUHTASARI WA MAENEO YA UTAWALA, MKOA WA SIMIYU
Katika muhtasari wa maeneo ya utawala, mkoa huu una halmashauri ambazo zimegawanyika katika mamlaka za miji na wilaya.

Idadi ya watu
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Simiyu ni 2,140,497; wanaume 1,034,681 na wanawake 1,105,816, ikiwa na wilaya 5.

Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi
Mkoa wa Simiyu una jumla ya majimbo ya uchaguzi Saba
  • Jimbo la Bariadi
  • Jimbo la Busega
  • Jimbo la Itilima
  • Jimbo la Meatu
  • Jimbo la Maswa Magharibi
  • Jimbo la Kisesa
  • Jimbo la Maswa Mashariki
ILIVYOKUWA UCHAGUZI MKUU 2020

Katika uchaguzi mkuu wa 2020 mkoa wa Simiyu, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipata ushindi mkubwa katika nafasi za urais, ubunge, na udiwani.

Kwa upande wa urais, mgombea wa CCM, Hayati John Pombe Magufuli, alipata kura nyingi dhidi ya mpinzani wake mkuu, Tundu Lissu wa CHADEMA.

Kwa nafasi za Ubunge, CCM ilifanikiwa kunyakua viti vyote katika majimbo 7

Uchaguzi wa Madiwani, (CCM) walipata ushindi mkubwa kwenye nafasi za madiwani ikifanikiwa kushinda kata nyingi. Hii ilitokana na upinzani kukumbwa na changamoto nyingi, zikiwemo wagombea wao kuenguliwa kutokana na matatizo ya kisheria au kutokidhi vigezo

Updates

January

February
March

ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
Back
Top Bottom