John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Picha: Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila mwanzoni kulia
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila ameagiza kupata maelezo ya kina juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi dhidi ya askari, Nuru Mtafya anayetuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi anayejulikana kwa jina la Neema Mabula wa shule ya sekondari iliyopo wilayani Maswa mkoani humo.
“Nataka kujua hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi dhidi ya askari, anayetuhumiwa kumpa ujauzito mtoto (Nuru Mtafya), baba yake amelalamika kwenye mkutano wangu wa hadhara kwa hiyo nahitaji majibu yakina katika hili," alisema David Kafulila.
Source: DarMpya