Simiyu: Mwanafunzi adaiwa kufariki kwa kuchapwa viboko na kukanyagwa kichwani na mwalimu shuleni

Simiyu: Mwanafunzi adaiwa kufariki kwa kuchapwa viboko na kukanyagwa kichwani na mwalimu shuleni

Shule za vijijini zina mateso sema kwa vile zijawahi kuchunguzwa.
 
Hayo ndo madhara ya kuajiri waalimu bila usaili
 
Jela zipi mkuu au hizi hizi za mama Abdul ambazo ikifika sikukuu ya muungano anatoka kwa msamaha wa mama Abdul. Chezea bongo nyoso veve
Tunafanyaje Sasa
Atawekwa hizi hizi ili nafsi zetu ziridhike tu japo haki kuipata ni geresha tu
 
Wazazi wa mwanafunzi Mhoja Maduhu wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mwasamba ya mkoani Simiyu wameomba uchunguzi ufanyike juu ya kifo cha mtoto wao kwa madai ya kuwa kifo chake kimesababishwa na kuchwapwa fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake akiwa shuleni.

View attachment 3258267
KIFO ni KIFO TU!

Tukutane kwenye sanduku la kura mwaka huu 2025.
 
Ndio maana inabidi walimu wafanyiwe udahili, tena wafanyiwe na tathmini ya afya ya akili maana Tanzania kuna vichaa wengi
 
Bado kuna walimu wanoshupaza shingo, baada ya matukio yote na maelekezo yote!.
 
Inaumiza sana mtoto kufa kifo cha kikatili namna hii.

Hivi walimu ni kwamba wana shida ya afya ya akili ama ni vipi?

Maana matukio kama haya yamekuwa yakujirudia karibu kila mwaka, licha ya walimu hao kufikishwa mahakamani na kufungwa lakini waliobaki huwa hawajifunzi.

Hivi mwalimu ukifundisha na kuondoka zako nyumbani pasipo kuchapa mtoto wa mtu unapungukiwa nini?

Au kuna posho walimu mnapewa pale ambapo mnaadhibu watoto?

Haya huyo mwalimu ndiyo kaaga mtaa kizembe hivyo anaenda jela na adhabu ya kuuwa ni kunyongwa hadi kufa.
 
Video inajieleza,ni mwalimu mwenzangu aliyekengeuka
Mimi kila mara huwa nawakumbusha walimu juu ya kuzingatia majukumu yao ya msingi na kuachana na hasira za kipumbavu za kuchapa watoto wasio na uwezo wa kujitetea.

Sasa kama huyu mwalimu ndoto zake zimeyeyuka kizembe sana anaenda jela maisha kisa kutokuwa na self control ya hasira za kipumbavu.

Bado nawashauri walimu watoto wa dunia ya leo watakupeleka jela kizembe sana maana afya zao sio imara kama walivyokuwa wa zamani miaka ya 80's na 90's.
 
Ww ni mwalimu?
 
Kumpiga fimbo kichwani na kumkanyanga kichwani siyo kwa mtoto hata mtu mzima anaweza kufa ukimfanyia hivyo.

Tujitahidi kuzuia hasira maana binadam kufa siyo kazi kubwa kama tunavyodhani, ni rahisi sana hasira za dakika 1 kukupeleka gerezani muda mrefu
 
Ww ni mwalimu?
Hapana. Ila nina marafiki na watu ninaofahamiana nao ambao ni walimu.

Kiukweli kuna wakati unajiuliza huyu naye amewezaje kuwa mwalimu?

Mtu ambaye tumeishi naye mtaani ni mtukutu tangu akiwa shule anavuta mibangi na mipombe halafu baadae unamkuta kaenda ualimu.

Huwa najiuliza kwamba ualimu ndiyo fani ambayo kila mtu anaiweza?

Kwanini wengi wao waliofeli kufikia ndoto zao za kitaaluma ndiyo hukimbilia ualimu?
 
Back
Top Bottom